Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella amekagua maendeleo ya utekelzaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Moivo.
Mradi unaotekelezwa na serikali kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Program ya Kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa Shule za Sekondari (SEQUIP), ikiwa ni utekelezaji wa makakati wa serikali wa kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ya sekondari.
Katika mradi huo licha ya mkuu huyo wa mkoa kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi huo, amewataka watalamu wa halmashauri kuzingatia hali ya ubora wa ujenzi unaofuata hatua na taratibu na kusistiza kuto kukimbizanan na dead line zaidi.
"Licha ya kwamba tunakimbizana na deadline ni vema kuzingatia viwango vya ubora wa ujenzi unaozingatia thamani ya fedha na ubora wa mradi 'value for money'" Amesisitiza Mhe. Mongella.
Msimamizi wa mradi na mkuu wa shule ya Enyoito, ameweka wazi kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba 8 Madarasa Maabara 3 za Sayansi, chumba cha Tehama, Maktaba, matundu ya vyoo vya wasichana na wavulana na chumba maalum cha wanafunzi wenye ulemavu, kichomea taka 1, mnara wa tank la maji lenye ujazo wa lita zaidi ya elfu 20
Awali Mkuu huyo wa mkoa, atafanya ziara tarehe 19 -20 .09.2023 ya kukagaua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu sekondari na Msingi, miundombinu ya barabara na maji, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero za wananchi katika kata za Oldonyowas na Bwawani.
Arusha DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.