Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa mabweni manne shule ya sekondari Mringa, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 100 kupitia program ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari (SEQUIP).
Mhe. Mongella, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendela kutoa fefha za kukarabati majengo kwenye shule kongwe za sekondari, licha ya kuhakikisha majengo yote yanakuwa kwenye hali nzuri ya ubora zaidi ni kuwawezesha watoto wa kitanzania kusoma na kufundishwa kwenye mazingira rafiki ili waweze kutimiza ndoto zao.
"Tunamshukuru sana Mhe Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ukarabati wa mabweni haya manne yaliyojengwa zaidi ya miaka 50, ambayo yatawawezesha wanafunzi kulala kwenye mazingira bora, mazingira ambayo licha ya kuchochea taaluma lakini pia yataimarisha afya za wanafunzi kwa kuwa na malazi mazuri.
Hata hivyo amemuagiza mkuu wa wilaya ya Arumeru kupitia Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha kufanya ukarabati wa jiko la
shule, ili liendane na hadhi ya majengo ya shule hiyo.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mkuu wa shule ya sekondari Mringa, Mwl. Salum Magaka amesema kuwa, wamepkea jumla ya shilingi milioni 360 kutoka serikali kuu, milioni 100 zikitumika kukarabati mabweni manne ya zamani
huku milioni 260 zikitumika kujenga mabweni mawili mapya yote ni maalumu kwa wanafunzi wasichana wa kidato cha tano na sita.
Hata hivyo Mwl. Magaka ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuijali na kuithamini shule hiyo kongwe kwa kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu kwa miaka mitatu mfululizo, shule ambayo inahitaji majengo zaidi kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi.
lMkuu huyo wa mkoa, atafanya ziara ya siku mbili 18 - 19.09.2023 ya kukagaua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu sekondari na Msingi, miundombinu ya barabara na maji, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero za wananchi katika kata za Oldonyowas na Bwawani.
Arusha DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.