Na Elinipa Lupembe
Walimu wametakiwa kuwasimamia wananfunzi kutunza vifaa vyote vya shule pamoja miundombinu iliyojengwa kwenye shule zao ili kwa paomja iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
Mhe.Mongella ameyasema hayo wakati akikagua ukarabati wa maabara ya somo la Kemia shule ya sekondari Mringa na kukuta baadhi ya mabomba yamevunjika.
Amesema kuwa walimu wanalo jukumu la kuwasimamia wanafunzi kutunza vifaa vyote vya shule na kuhakikisha vinakuwa kwenye hali nzuri wakati wote kwa kuwa ndivyo vinavyowasaidia katika masomo yao na kuongeza kuwa kufanyiwa matengenezo kwa haraka pindi unapotokea uharibifu.
"Fanyeni utaratibu mzuri wa utunzaji wa vifaa vya shule kwa wote walimu na wanafunzi, kuweni na desturi ya pindi kifaa kimeharibika mwalimu wa somo na mkuu wa shule hakikisha kinafanyiwa matengenezo kwa haraka badala ya kusubiri viharibike vyote, jambo ambalo litahitaji fedha nyingi zaidi" Amesisitiza Mhe. Mongella.
Ameongeza kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kujenga na kununua vifaa vya kujifunzia, fedha ambazo ni kodi za wananchi,hivyo kila mwenye dhamana atimize wajibu wake kwa kuhakikisha vifaa vyote vinatunzwa ili vitumike kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Ametolea mfano wa mabweni yaliyojengwa miaka 50 iliyopita ambayo yanafanyiwa ukarabati, na kuweka wazi kuwa yasingetunzwa na watungulizi wetu, tusingeyakuta ni vema kuweka uzalendo mbele wa kutunza mali ya Umma
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA✍✍
#kaziinaendela✍✍
PICHA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.