RCC YAPOKEA OMBI NA PENDEKEZO LA KUFUTA MAMLAKA YA MJI MDOGO NGARAMTONI
Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kimepokea mapendekezo kutoka Halmashauri ya Arusha yaliyojielekeza kufutwa kwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni kutokana na gharama kubwa za uendeshaji,Kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Desemba 18, 2024.
Akiwasilisha mapendekezo hayo kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, bwana Suleiman Msumi, amesema uamuzi huo unatokana na malalamiko ya wananchi ambao kwa muda mrefu wamedai gharama ya huduma za uendeshaji wa Mamlaka ya mji mdogo kuwa kubwa.
Amesema malalamiko hayo yalitolewa kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara ikiwemo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Chtistian Makonda aliyembatana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa (CCM) kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi,ambapo mionhoni mwa kero, wananchi walilalamikia gharama kubwa uendeshaji wa Mamlaka ya mji mdogo na kuomba ifutwe.
Aidha, amebainisha kuwa, Halmashauri ilipokea malalamiko ya wananchi ambao walionyesha kuwa hawako tayari kuwepo kwa Mamlaka hiyo na kulazimu Halmashauri kuanza mchakato wa vikao vya maoni kuanzia ngazi za vijiji na hatimaye kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya fedha na Baraza la Madiwani na hatimaye kufikishwa kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya (DCC)
Msumi ameendelea kueleza kuwa, baada ya vikao hivyo kutoa pendekezo hilo, halmashauri imewasilisha kwenye kikao Kamati ya Ushauri Mkoa ili kuwasilisha ombi hilo Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI )kwa hatua zaidi.
Akichangia hoja hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mhe. John Maha, ameomba halmashauri zao zipandishwe hadhi na kuwa manispaa kwa kuwa kuna faida zikipandishwa hadhi na kuwa manispaa.
Ameshauri iundwe Kamati ya Mkoa itakayokuwa ikipendekeza halmashauri kupandishwa hadhi na kuongeza kuwa hata Karatu nao wana Mamlaka ya mji mdogo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.