Na Elinipa Lupembe
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha imetoa salamu kwa Wajumbe wa Baraza la Madiwani, halmashauri ya Arusha, wakati wa mkutano wa kujadili taarifa za robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akitoa salam hizo kwa niaba ya RAS mkoa wa Arusha, CPA. Ramadhani Madegeka ameeleza kuwa, kama ilivyo malengo ya mkoa ni ukusanyi wa mapato, madiwani na wataalamu mnatakiwa kushirikiana katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, halamshauri na mkoa uweze kufikia malengo tuliyojipangia kwa mwaka.
"Bila kukusnaya Mapato hatutaweza kufikia malengo tuliyojipangia, niwatake waheshimiwa kuonheza nguvu kayika ukuapsanyaji wa mapato, hadi kufikia mwezi Oktoba, halmashauri imekusanya shilingi bilioni 1.2 sawa na asilimia 26 kutoka kwenye makisio ya shilingi bilioni 4.8 kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ili kufikia 100 % lazima nguvu iongezeke".
Aidha amewataka waheshimiwa Madiwani kushiriki katiaka usimamizi wa miradi ya maendeleo, kwa kuwa kwa robo ya kwanza serikali kuu imetoa fedha nyingi za kutekelza miradi pamoja na asilimia 40 ya mapato ya ndani, hivyo madiwani mnawajibu wa kuzisimamia fedha hizo na miradi iweze kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaoendana na thamani ya fedha.
Mkoa unasisitiza kushitikiana kwa pamoja watalamu, madiwani na wananchi kwenye usimamizi wa miradi, kwa taratibu za matumizi ya force akaunti.
Serikali imetoa fedha za nje ya bajeti, milioni 760 za ujenzi wa madara 38 ya kidato cha kwanza mwaka 2023, madarasa yanatarajia kukamilia mwanzoni mwa mwezi Disemba, ushiriki wa madiwani ni wa muhimu sana"Amesisitiza Madegeka
Aidha amewataka madiwani kuzingatia suala la utawala bora kwamba kila Diwani anatakiwa kufuatilia mipango yote na utekelezaji wake na kuhakikisha kila kilichopangwa kufanyika kifanyike kulingana na bajeti iliyopangwa
Madiwani mnatakiwa kuzingatia mgawanyo wa matumizi kulingana na kanuni za matumizi ya mapato ya ndnai ya asilimia 40 utekelzaji wa miradi, asilimia 10 za mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu,na asilimia 50 ya matumizi ya kawaida, ili kuepeuka migogoro isiyokuwa ya lazima na matumizi yasiyozingatia sheria.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.