Shirika la kimataifa la WaterAid Tanzania limewakutanisha wadau mbalimbali kwenye Ukumbi wa Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela kwa ajili ya semina elekezi kwa lengo la kuwaweka wazi wadau watakao husika katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaotegemea kuanza kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha 2017/18.
Mradi huo wa maji tayari umeanza kwa kufanya upembuzi yakinifu na unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID) utakao gharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 1.6 sawa na fedha za Tanzania shilingi 426,607,17.00 kwenye kata za Lemanyata, Olkokola na Oltrumet halmashuri ya Arusha
Mkurugenzi wa Shirika la WaterAid Tanzania Dk. Ibrahimu Kabole amesema lengo la semina hiyo elekezi ni kuutambulisha mradi huo kwa wadau ili kuwa na uelewa wa pamoja kwa wahusika wote wataoshiriki katika kutekeleza mradi pamoja na kufahamu gharama za mradi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.