SERIKALI KUTOA WARAKA KWA AJILI YA WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU
Serikali inatarajia kutoa waraka utakao waelekeza wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutekeleza miongozo inayowahusu watumishi wa Umma wenye ulemavu ili wapate mazingira rafiki na wezeshi wanapotekeleza majukumu yao.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 06,2025 Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zaina Katimba alipomwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa katika ufunguzi wa kikao cha wajumbe wa baraza la Taifa wa Chama cha Walimu Tanzania ambao ni wawakilishi wa walimu wenye Ulemavu.
“Serikali itatoa waraka kuwakumbusha wakurugenzi wote nchini kutekeleza miongozo
inayowahusu watumishi wa umma wenye ulemavu na niziombe taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa kuendelea kufanikisha upatikanaji wa vifaa visaidizi kwa watumishi wa umma na wanafunzi wenye ulemavu” Amesema
katika hatua nyingine Mhe. Katimba amewakumbusha viongozi wa vyama vya siasa kutoa nafasi kwa watu wenye Ulemavu wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili waingie kwenye vyombo vya maamuzi kwa ustawi na maendeleo ya watu wenye ulemavu na taifa kwa ujumla.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.