SERIKALI YA AWAMU YA SITA ILIVYOIPAISHA SEKTA YA AFYA NCHINI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko leo tarehe 25 Aprili,2025 amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha na kujiona jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya afya nchini huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya uongozi thabiti chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Biteko ameyasema hayo alipotembelea na kukagua mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri ya Meru iliyopo Tengeru Wilayani Arumeru ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwa baadhi ya Wilaya Mkoani Arusha.
Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kupongeza thamani ya fedha za umma zilivyotumika kwa ufanisi huku akisisitiza kuwa huduma bora kama hizo ni matokeo ya mipango madhubuti ya Serikali ya awamu ya sita.
“Huduma bora namna hii siyo bahati mbaya, ni matokeo ya uongozi makini na maono ya mbali ya Rais Samia. Hapa tumeona ubora ukizingatiwa sambamba na thamani ya fedha zilizotumika”. Amesema.
Sambamba na hilo,Dk.Biteko amesisitiza umuhimu wa kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kuwanufaisha jamii kwa muda mrefu na pia akatoa wito kwa wananchi kudumisha mshikamano wa Kitaifa kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisi na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume Rais wa Kwanza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, amesema kuwa Mkoa Arusha umeandaa mkakati wa kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuanzisha ushirikiano wa kimatibabu na utaalam toka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwapunguzia wananchi gharama kubwa za matibabu.
“Tunalenga kuwa na hospitali moja maalum ya rufaa itakayoshirikiana na madaktari bingwa kutoka nje ya nchi na ndani ili kutoa huduma bora kwa wananchi wetu hasa wale wa kipato cha chini waweze kunufaika na huduma hiyo ya matibabu.” Amesema Mhe. Makonda.
Mradi huo umetekelezwa kwa 'force account' kwa gharama ya shilingi milioni 900 zilizotolewa na Serikali Kuu, na hadi sasa umekamilika kwa asilimia 100, hivyo kuongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma bora kwa wananchi.

Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.