Na Elinipa Lupembe.
Serikali imeendelea kutekelea mkakati wa kuboresha miundombinu ya shule nchini, kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 589.5 za ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari halmasahuri ya Arusha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, ofisini kwake mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi amethibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa majengo ya shule, lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto wa kitanzania anapata elimu katika mazingira bora
Msumi ameweka wazi mchanganuo wa fedha hizo ni pamoja na milioni 180 ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa, milioni 400 ujenzi wa nyumba 4 za walimu wa shule za msingi, milioni 87.5 ukamilishaji wa vyumba 7 vya madarasa na milioni 30 ujenzi wa uzio shule ya msingi Ilboru.
Milioni 22 ujenzi wa matundu 20 ya vyoo shule 3 za msingi, milioni 50 ukamilishaji wa vyumba 4 vya maabara shule mbili za sekondari za Olomitu na Kiserian, pamoja na milioni 20 kutumika kukamilisha ujenzi wa bweni shule ya sekondari Oldadai.
Hata hivyo, mkurugenzi Msumi ameipongeza serikali kwa ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu kwa shule za pembezoni, maeneo ambayo walimu wanateseka kwa kukosa mahali pa kuishi kutokana na maeneo hayo kukosekana kwa nyumba za kupangisha.
"Ninampongeza na kumshukuru mheshimiwa Rais, mama Samia, kwa kuwakumbuka walimu wa shule za pembezoni, shule zile zina idadi ndogo ya walimu kwa kuwa hakuna mahali pa kuishi, kutokana na asili ya makabila ya kimaasai, hakuna nyumba za kupangisha, uwepo wa nyumba za walimu, unatoa fursa kwa walimu kupata mahali pa uhakika pa kuishi katika eneo la shule". Amefafanua Mkurugenzi Msumi.
Naye Mkuu wa Idara ya Mipango, halmashauri ya Arusha, Anna Urio, amesema kuwa fedha hizo tayari zimeingia kwenye akaunti za shule, miradi yote itatumia mafundi wazawa 'force account', na tayari taratibu za utekelezaji wa miradi yote zimeanza na miradi hiyo inayegemea kukamilika kwa muda wa miezi 3.
"Tumeshawapa maelekezo wasimamizi wa miradi hiyo, ambao ni walimu, taratibu zote za utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo, matumizi ya 'Force Account' namna ya kupata wakandarasi na wazabuni, uteuzi wa kamati za usimamizi, pamoja na kuzingatia 'value for money' katika miradi yote". Amefafanua Afisa Mipango huyo
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Salvatory Alute, amebainisha kusimamia miradi hiyo ambayo ikio chini ya mamalaka ya yake na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya ubora unaoendana na thamani ya fedha.
"Inafahamika uwepo wa miundombiu bora shuleni, unaongeza ari ya wanafunzi kujifunza na kupenda shule, sambamba na walimu kufundisha katika mazingira rafiki, miundombinu hii itapandisha taaluma ahuleni na kuongeza ufaulu" Amesisitiza Afisa Elimu huyo.
Ikumbukwe kuwa Serikali tayari imeanza utekelezaji wa bajeti ya miradi ya maendeleo ya mwaka mpya wa fedha 2022/2023, kwa kutoa kiasi hicho cha fedha, ikiwa ni utekezaji wa miradi ya mwaka huo wa fedha katika sekta ya elimu.
ARUSHA DC TUPO KAZINI
KAZI INAENDELEA✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.