Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho kwenye utoaji wa mikopo ya asilimia 10% kwa makundi ya Vijana,Wanawake na Watu wenye Ulemavu,ambapo kwa upande wa Vijana maboresho ya umri yemezingatiwa kutoka miaka 35 mpaka 45.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi na utoaji wa Mikopo kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mkuu wa Wilaya Arumeru Amir Mohamed Mkalipa alisema kuwa Serikali inayoongozwa na Dr.Samia Suluhu Hassan imesikia kilio cha Vijana wengi hususan kwenye kigezo cha umri kilichokuwa kizuizi kikubwa kwa vijana kutumia fursa hiyo yakujinufaisha na mikopo hiyo.
Aidha,Mh Mkalipa aliongeza kwa kusema kuwa kazi kubwa kwa vikundi vilivyokidhi vigezo ni kuhakikisha vinatumia vizuri fursa hiyo ili kujikwamua kiuchumi na pia vizingatia makubaliano ya kisheria katika kurejesha mikopo hiyo kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha ndugu Suleiman Msumi akimkaribisha Mkuu wa Wilaya wa Arumeru Mhe.Mkalipa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo, alisema kuwa Halmashauri ya Arusha kwa awamu hii itatoa mikopo yenye thamani ya milioni 982 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na wetu wenye Ulemavu.
Msumi aliongeza kwa kusema kuwa kiasi hicho cha shilingi milioni 982 kitagawanywa kwa makundi matatu ikiwa shilingi milioni 392,854,932 zitatolewa kwa Vikundi vya Wanawake ambapo ni sawa na asilimia 40%,huku shilingi milioni 392,854,932 sawa na asilimia 40% kitatoewa kwa vikundi vya Vijana na shilingi milioni 196,427,466.25 sawa na asilimia 20% zitatolewa kwa kundi la Watu wenye Ulemavu.
Aidha Halmshauri kwa siku ya leo tarehe 25/10/2024 imetoa fedha kiasi cha Shilingi milioni 792,952,500, Wanawake shilingi 390,912,000, Vijana wamepokea kiasi cha shilingi 363,040,500 na Watu wenye Ulemavu wamepokea kiasi cha shilingi 39,000,000. Fedha hizo ni kwaajili ya miradi yasekta ya Kilimo na Mifugo,usafirishaji na biashara.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.