• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANAFUNZI 156 WAMEPANGIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 SHULE YA SEKONDARI LIKAMBA

Posted on: January 6th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Jumla ya wanafunzi 156 wavulana 77 na wasichana 89 wamepangiwa kuanza kitado cha kwanza shule ya sekondari Likamba muhula wa masomo unaonza Januri 9, 2023 na kuifanya shule hiyo kuwa na jumla ya wanafunzi 358.

Mkuu wa shule ya Sekondari Likamba, Mwl. Richard Mugyabuso amethibitisha kuwa, idadi hiyo ya wanafunzi inakwenda sambamba na uwepo wa vyumba vya madarasa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tatu shuleni hapo.

Amesema kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule ambayo inakua kwa kasi kutokana na ukweli kwamba, serikali inaendelea kuongeza nguvu kwa kuimarisha miundo mbinu yake ili iweze kukidhi mahitaji ya wanafunzi kwa ujumla wake.

Mwaka 2019 wananchi wa kijiji cha Likamba waliamua kuunganisha nguvu na kuanza mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya Sekondari Likamba,  kutokana na Jiografia ya kata ya Musa, ilionekana bado  watoto wa kijiji cha Likamba walitembea umbali mrefu kufika shule ya kata ya sekondari ya Musa.

Wananchi hao walikusanya pesa na kufanikiwa kujenga vyumba 4 vya madarasa, matundu 8 ya vyoo pamoja na nyumba moja yenye uwezo wa kuishi  walimu 8 japokuwa bado hazijakamilika.

Baada ya serikali kuziona juhudi hizo za wananchi hao, ilianza kuweka nguvu kwa kusajili shule hiyo kwa namba S.5349 na hatimaye Januari mwaka 2020, shule ilianza  kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Mwaka wa fedha 2020/2021 na 2021/2022 serikali kupitia mradi wa EP4R ilijenga madarasa 4 na baadaye kujenga darasa 1 kwa fedha za mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Hata hivyo wananchi wa Likamba  walianzisha mradi wa ujenzi wa maabara na baadaye serikaki kukamilisha maabara ya masomo ya Sayansi.

Licha ya mafanikio hayo yote, mwishoni mwa mwaka 2022 serikali pia imetoa shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa, viti na meza 50 kwa kila darasa ikiwani maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2023.

Ikumbukwe kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ni utelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 79 kifungu (q) Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za Msingi na Sekondari nchini.


ARUSHA DC

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.