Mkoa wa Arusha umepewa heshima ya Kitaifa ya kuwa mwenyeji wa sherehe kubwa ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zitakazofanyika Machi 8, 2025, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo " Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki,Usawa na Uwezeshaji" yanalenga kuhamasisha usawa wa kijinsia na kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika nyanja mbalimbali za jamii.
Aidha, maadhimisho hayo pia yatachagizwa na wiki ya michezo ya aina mbalimbali, ikiwemo mechi za mpira wa miguu kati ya timu maarufu za wanawake, Simba Queens, Yanga Queens, JKT Queens na Fountain Gate FC, ili kusherehekea ushiriki wa wanawake katika michezo.
Kwa mara ya kwanza, maadhimisho haya yatakuwa ya kipekee, ambapo sherehe zitaanza tangu Machi 1, 2025, na kudumu kwa siku saba, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Mwanamke. Katika kipindi hicho, wizara nane zitatoa huduma muhimu kwa jamii, ikiwa ni pamoja na huduma za afya, kisheria, na elimu ya fedha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.