• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Shilingi bilioni 50.8 zakadiriwa kukusanywa na kutumika 2019/2020

Posted on: January 25th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Wajumbe wa Baraza la madiwani, halmashauri ya wilaya ya Arusha, wilayani Arumeru wamepitisha rasimu ya makadirio ya mpango wa bajeti wa mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha 2019/2020, huku asilimia 15 ya bajeti hiyo ikijikita kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha rasimu hiyo ya mpango wa bajeti, katika mkutano maalumu wa baraza la madiwani, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, ameeleza kuwa, katika mwaka wa fedha ujao wa 2019/2020, halmashauri ya Arusha imekadiria kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi bilioni 50.8, huku bajeti hiyo ikijikita kwenye ukomo ule ule wa makisio ya mwaka wa fedha 2018/19, kukiwa hakuna ongezeko lolote la fedha.

Mkurugenzi huyo, ameainisha mchanganuo wa makadirio hayo ya mapato na matumizi wa bajeti hiyo, kwa kuwaelezea wajumbe kuwa, kiwango hicho cha fedha kitatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo, mapato ya ndani, mishahara pamoja na miradi ya maendeleo na kuweka bayana kuwa, kiasi cha shilingi bilioni 1.3 sawa na asilimia 2.92 kitatokana na mapato ya ndani, Ruzuku fidia ya mapato imekadiriwa jumla ya shilingi milioni 58 sawa na asilimia 0.16, Ruzuku ya matumizi mengine shilingi bilioni 1.5 sawa na asilimia 2.92.

Ameendelea kufafanua kuwa, kiasi cha shilingi milioni 39.9 sawa na asilimia 78.38 ikiwa ni Ruzuku ya mishahara  na kiasi cha shilingi milioni 38.3 sawa na asilimia  0.08 ikiwa ni mishahara itakayotokana na mapato ya ndani, huku kiasi cha shilingi bilioni 8.07 sawa na asilimia 15 kikielekezwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kwa mwaka wa fedha 2019/2020, halmashauri inategemea kutumia kiasi cha shilingi bilioni 8.07, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 3.6 ikiwa ni mchango wa halmashauri kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani na kiasi cha shilingi bilioni  4.3 ikiwa ni Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu.

Dkt. Mahera ametaja mchanganua wa makadirio ya fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi bilioni 8, kuwa ni pamoja na kiasi cha shilingi milioni 56.3 ikiwa ni fedha za Mfuko wa Jimbo sawa na asilimia 0.70, shilingi milioni 605.2 Mfuko wa afya wa pamoja - HSBF sawa na asilimia 7.50, shilingi bilioni 1.4 fedha za Ruzuku ya kuendeleza maji vijijini-NWSSP sawa na aslimia 17.66, Ruzuku ya elimu bila malipo kwa shule za Msingi shilingi milioni 831 sawa na asilimia 10.30, ruzuku ya elimu bila malipo sekondari shilingi bilioni 1.4 sawa na asilimia 17.72, shilingi  milioni 45 fedha za kampeni ya Usafi wa Mazingira sawa na asilimia 0.56 huku shilingi bilioni 3.6 sawa na asilimia 45.67 ikiwa ni fedha za Mapato ya ndani.

Aidha Mkurugenzi Mahera amesisitiza kuwa, katika rasimu ya bajeti ya  mwaka wa fedha 2019/2020, halmashauri imepanga kutekeleza majukumu yake ya msingi yenye lengo la kutoa huduma bora na kuondoa umasikini kwa wananchi wake kupitia vipaumbele vyake kwa kushirikiana na wananchi, Serikali kuu na wadau wa maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, kilimo na ushitika, mifugo na uvuvi, ardhi, maliasili na mazingira, rasilimali watu na TEHAMA.

Licha ya halmashauri kukabiliwa na changamoto kubwa katika ukusanyaji wa mapato,halmashauri imejipanga kubuni vyanzo vipya vya mapato huku ikiendelea kushirikisha jamii katika ulioaji wa kodi na ushuru mbalimbali.

Hata hivyo, baada ya mjadala mrefu na wa kina, wajumbe wa baraza la madiwani, wameridhia mapendekezo ya rasimu hiyo ya mpango wa makadirio ya mapato na matumizi yaliyowasilishwa, kutokana na uhalisia wa bajeti hiyo kujikita kwenye sekta zote,zaidi ikielekeza kujikita katika kutoa huduma bora kwa jamii na kuondoa umasikini na kuahidi kutoa ushirikia kwa watalamu katika kutekeleza bajeti hiyo.

Diwani wa kata ya Musa, mheshimiwa  Flora Zelote amesema kuwa, mapendekezo ya rasimu ya bajeti yanaridhisha kwa kuwa umbile la bajeti limegusa maslahi mapana ya jamii hususani afya, elimu, usalama wa raia na miundombinu na haki za binadamu.

Mara baada ya rasimu hiyo kupitishwa, halmashauri imeahidi kutekekeleza bajeti hiyo kwa kuzingatia maslahi mapana ya wananchi na kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kutumia mashine za kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.