Na Elinipa Lupembe.
Shirika la Builders of Future Africa linalofanya kazi mkoani Arusha limetambulisha mradi wa kuwahudumia kinamama wadogo 'early mothers' kwenye kata tatu za halmashauri ya Arusha, mradi unaotarajiwa kurejesha ndoto zilizotoweka za kina mama hao.
utakaogharimu shilingi milioni 34.5.
Akizungumza wakati wa kikao cha kutambulisha mradi huo, kilichofanyiaka kwenye ukumbi wa mikutano halmasahuri ya Arusha, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu, halmashauri hiyo, Elizabeth Ngobei kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amesema kuwa mradi huu unakwenda kurejesha ndoto na matumaini ya wasichana waliopata mimba za utotoni na kurudi kwenye maisha ya kawaida.
Ameongeza kuwa, mradi huu ni muhimu kwa vijana ambao, waliingia kwenye kadhia ambayo hawakutarajia, na jamii imeonekana kushindwa kukubaliana na uhalisia, jambo ambalo limesababisha wengi kukata tamaa na wengine hata kuchukua maamuzi magumu ya kujiua.
"Ninaamini mnakwenda kufanya kazi ambayo, matokeo yake yatakuwa na manufaa kwa wasichana na watoto wao, kwa familia, kwa jamii na Taifa kwa ujumla, tekelezeni mradi kama ulivyokusudiwa na hakikisheni mnatoa taarifa kwa kila tobo ya mwaka kama taratibu za serikali zinavyoelekeza". Amefafanua Elizabeth
Akitambulisha mradi huo, Mkurugenzi wa shirika la BFA, Elisante Ephrahim amesema kuwa kwa awamu ya kwanza mradi huo utagharimu shilingi milioni 34.5 na utajihusisha na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa kina mama hao, pamoja na kuwafanya kujitambua na kujithamini.
Amefafanua kuwa shirika limefikia kutekeleza mradi huo, kutokana na changamoto iliyokuwa ikiwakabili wasichana waliopata mimba za utotoni na kujikuta yakipoteza mwelekeo wa maisha kutokana na kutengwa na familia na jamii, huku ndoto zao kiwa zimeyeyuka.
"Mradi huu unakwenda kurejesha ndoto za kina mama wadogo, kwa kuwajengea uwezo na kuwapa ujuzi na maarifa ya kurejesha matumaini yaliyopotea, ndani ya jamii zetu wasichana waliopata mimba za utotoni, hupitia ukatili na kutegwa na jamii zao, hali inayosababisha kukataa kwa kukatisha ndoto pasi kutegemea". Amefafanua Ephrahim
Mafunzo hayo yatawaunganisha kina mama hao kwenye vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kuanzisha biashara zao kulingana na matakwa yao ili waweze kujikwamu akiuchumi lakini kukabiliana na hali ya ukatili waliupata katika kipindi cha mimba za utotoni.
Hata hivyo madiwani wa kata hizo, wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo katika maeneo yao, huku wakilipongeza na kulishukuru shirika hilo kwa mradi huo, wakiamini ukifanyika kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa utakwenda kuzaa matunda kwenye jamii zao.
Diwani wa kata ya Mwandeti Mhe. Logolie Lukumay amekirinkuwepo kwa changamoto ya ndoa za utotoni katani mwake hususani kijiji cha Engalaoni na kuongeza kuwa anatamani mrafi huo utekelezwa kwa ukubwa zaidi ili kuwanusuru kina mama hao wadogo pamoja na wachana wanaoendelea kukua.
Naye Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali, halmashauri ya Arusha, Ahadi Mlay amelipongeza shirika hilo kwa kufuata taratibu zinatakiwa na serikali na kuyataka mashirika mengine kuiga mfano huo kwa kuwa kazi zote zinatekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele vya serikali hususani kwenye uwazi katika utekelzaji wa miradi.
"Niwatake mashirika yote kuzingatia taratibu zote kushindwa kufanya hivyo, shirika litakosa sifa na kufutiwa usajili jambo ambalo halipaswi kutokea, kwa kuwa serikali inawategemea mashirika kuwahudumi wanachi, hakikisheni miradi yote na gharama zake zinafahamika maeneo husika kwa uwazi" Amesisitiza Ahadi
Awali mradi huo wa nguvu ya binti rika na mama wadogo unategemea kuwafikia wamama wenye watoto 350, na kufanyika kwa miezi 6 kwenye kata za mwandet, Lemanyata Lengijave.
ARUSHA DC
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.