Na Elinipa Lupembe
Shirika la CCBRT kanda ya Moshi wametoa viti mwendo 17 kwa watoto 17 wa shule ya msingi na awali,wenye ulemavu wa viungo halmashauri ya Arusha.
Akizungumza wakati wa kukabidhi viti mwendo hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa, amewashukuru wadau wa shirika la CCBRT kwa msaada huo muhimu na wathamani kwa watoto wenye ulemavu.
Ameongeza kuwa licha ya watoto hao wana na changamoto lakini wazazi wenye watoto wenye ulemavu wanapitia changamoto nyingi zaidi katika malezi hivyo jamii inatakiwa kuungana kutoa msaada wa hali na mali pamoja na kuwatia moyo familia zenye watoto hao.
"Tunalo jukumu kubwa la kuwahudumia watoto wenye ulemavu, kila mtu anayo nafasi kubwa ya kufanya jambo kwa familia hizi kwa kuwa changamoto ya malezi ya watoto hawa ni zaidi ya maisha ya kawaida ya binadamu, tutumie muda hata kuwatia moyo" Amesema Mhe. Mwenyekiti huyo.
Aidha ameipongeza serikali kwa kuweka mazingira bora kwa wadau wa maendeleo na kuwa serikali inathamini kazi kubwa inayofanya na wadau na kuwataka kuendelea kuisaidia serikali katika kuhudumia jamii hususani watoto wenye mahitaji maalum
Naye Mratibu wa Huduma za Viti mwendo CCBRT Moshi, Neophita Lukiringa amesema kuwa, lengo la shirika kutoa msaada huo ni kwasaidia watoto kuweza kwenda shuleni na kufikia ndoto zao za kielimu lakini pia kuwasaidia wazazi kurahisisha kazi ya kuwahudumia watoto hao.
Hata hivyo wazazi na watoto waliopewa viti hivyo wameshukuru kwa msaada huo, ambao wamekiri ni huduma ambayo walemavu wengi wanaihitaji kwa ajili ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Fatuma Yusuph mama Sahil mtoto wa miaka 9, licha ya kushukuru ameitaka jamii kuendelea kuwasaidi wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwa malezi ya watoto hayo yana gharama kubwa na zaidi yanahitaji mzazi kutumia muda wote bila kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.
"Mtoto wangu ana miaka 9 sasa, nahitajika muda wote kuwa nae karibu, ili kumuhudumi, kiwa na kiti mwendo kutanipunguzia kidogo kazi na mimi kupata muda wa kufanya majukumu mengine". Amesema Fatuma
Naye Rachel Mollel mtoto aliyepewa kiti ameishukuru serikali kwa msaada huo, na kuweka wazi kuwa kiti hicho kitamsadia kutembea akiwa shuleni na nyumbani pia.
Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Selema Msumi, licha ya kushukuru kwa msaada huo, amesema kuwa halmashauri ina watoto 509 wenye uhitaji ambao wanasoma kwenye shule zenye vitengo maalum huku watoto 77 wakisoma kwenye shule ya bweni Ilboru hivyo mahitaji ya watoto hao ni mengi kulingana na idadi yao.
Awali uongozi wa licha ya kuwashukuru wadau, unawataka wadau kuendelea kujitokeza kuchangia maendeleo ya jamii katika halmashauri hiyo.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
#kaziiendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.