• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHIRIKA LA GLAMI LAKABIDHI JENGO LA CHOO CHA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI MRINGA

Posted on: February 13th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Shirika La Girls LiveliHood & Mentorship Initiative  'GLAMI', limekamilisha na kukabidhi mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya choo cha wasichana chenye matundu 10, mradi uliogharimu shilingi milioni 22.2 kwa shule ya sekondari Mringa.

Akikabidhi mradi huo, Mkurugenzi wa Miradi  shirika la GLAMI, Asimwe Sued, amesema kuwa, shirika hilo, limejenga miundo mbinu hiyo ya choo cha kisasa, lengo likiwa kuwasaidia na kuwawezesha wasichana kusoma kwa amani na utulivu, hasa kwa kuzingatia changamoto za kiafya na kimazingira zinazoathiri  wasichana kwenye masomo yao, wakati wakiwa kwenye hedhi.

Ameongeza kuwa, wasichana wanapata changamoto kubwa wakati wa hedhi wawapo shuleni, kwa kukosa sehemu za kujisitiri kutokana na shule nyingi kukosa miundo mbinu hiyo, hivyo shirika limeona ni vyema kuungana na serikali kwa kujenga miundo mbinu ya choo, yenye sehemu ya kubadilishia taulo wakati wakiwa kwenye hedhi.

"Shirika limezingatia, Hedhi Salama kwa watoto wa kike wawapo shuleni, lengo ni kuwawezesha wasome kwa amani na kuhudhuria masomo yao, bila kukosa vipindi kwa sababu ya hedhi na zaidi waweze kufikia malengo na kutimiza ndoto zao" amesema Mkurugenzi Asimwe.

Hata hivyo Mkurugenzi Asimwe, ameweka wazi miradi inayotekelezwa na shirika hilo katika halmashauri ya Arusha, miradi miwili  ya KISA  na BINTI SHUPAVU na kufafanua kuwa mradi wa KISA, unaotoa mafunzo ya uongozi na stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha tano na cha sita huku mradi wa  BINTI SHUPAVU, ukitoa mafunzo ya uongozi binafsi na stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, amepokea mradi huo  kwa kuwashukuru wadau hao wa maendeleo wa shirika la GLAMI, kwa msaada huo, na kuthibitisha kuwa uwepo wa miundo mbinu ya choo cha kisasa chenye sehemu ya kujistiri wasichana wakati wa hedhi, licha ya kuhakikisha afya za watoto hao, lakini itaongeza mahudhurio kwa wasichana na kupandisha taaluma kwa wasichana hao.

"Tunafahamu wasichana wengi hukosa masomo, kipindi cha hedhi, takwimu zinaonyesha, mtoto wa kike hushindwa kuhudhuria vipindi 3-4 kwa mwezi, vipindi 48 kwa mwaka wakati wa hedhi, uwepo wa miundo mbinu hii, utaongeza siku za msichana kuhuduria masomo bila kukosa, niwasihi kuvitunza vyoo hivi kwa kuwa, wafadhili wametumia fedha nyingi, kujenga" ameweka wazi Mkurugenzi Msumi

Naye mkuu wa shule  sekondari Mringa, Mwalimu Salim Magaka, licha ya kulishukuru shirika hilo kwa kujenga miundombinu ya vyoo vya wasichana shuleni hapo, amesema kuwa, miundo mbinu hiyo imejengwa wakati muafaka kutokana na ukweli kwamba, shule ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo, hasa ulinganisha na idadi  kubwa ya wanafunzi shuleni hapo, choo hicho kitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi hasa wa kike.

Aidha amepongeza pia uwepo wa choo cha kisasa chenye miundo mbinu ya kujisitiri watoto wa kike jambo ambalo, ilikuwa ni changamoto kubwa shuleni hapo, na kuongeza kuwa, anaamini changmoto ya wasichana kushindwa kuhudhuria masomo wakati wa hedhi itapungua kwa kiasi kikubwa.

Awali halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na  shirika la GLAMI linatekeleza miradi yake ya Kisa na Binti Shupavu kwenye shule 10 za sekondari za  Mringa, Mwandet, Mlangarini, Enaboishu na Cornerstone, pamoja na  mradi wa Kisa kwenye shule za sekondari Mukulat, Einoth,Kimnyaki, Mateves, Mwandet na Ilkidin'ga.

ARUSHA DC

KaziInaendeleaaa...✍✍✍







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.