• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHIRIKA LA HAND IN HAND EASTERN AFRICA TZ, LATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA UVIKO 19, ARUSHA DC

Posted on: August 6th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Shirika lisilo la kiserikali la Hand in Hand Eastern Africa Tz, limetoa msaada wa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19, kwenye kata sita  za pembezoni, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, maeneo ambayo shirika hilo linafanya kazi za kijamii na wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, mkurugenzi wa shirika hilo, Bi.Jane Sabuni, amesema kuwa shirika  limefikia hatua hiyo, baada ya kushuhudia vifo vinavyotokana na UVIKO 19, ndani ya familia na jamii kwa ujumla, na kuona umuhimu wa uwepo wa  vifaa vya kujikinga na UVIKO 19,  kwa jamii zinazoishi maeneo ya vijijini, kutokana na ukweli kwamba kuna ugumu katika upatikanji  vifaa kinha hivyo kutokana na umbali wa kufuata vifaa hivyo mijini.

Mkirugeznzi Jane amefafanua kuwa, shirika lao linafanya kazi ya kuwajengea uwezo wananchi juu ya ujasiriamali,  hivyo ili wananchi hao wafikie malengo yaliyokusudiwa ni lazima wawe na afya bora, na ili kuwa na afya ni lazima kujikinga  na UVIKO 19, kwa kunawa mikono kwa  sabuni na maji tirirka pamoja na kuvaa barakoa wakati wa kufanya shughuli zao, hasa  kwenye mikusanyiko ya watu wengi.

"Shirika linafanya kazi na wajasiriamali ambao wako kwenye risk kubwa ya kupata maabukizi ya UVIKO 19, kutokana na maeneo ya mikusanyiko wanayofanyia shughuli zao za kila siki, ili kuwaepusha kupata maambukizi, shirika limetoa matanki ya kunawaia  mikono, sabuni za maji pamoja na barakoa, lengo likiwa ni kusaidia wadau wetu kujinga na UVIKO 19, waweze kufikiammalengo yao." Ameweka wazi Mkurugenzi Jane.

Naye Kaimu Mkurugenzi, Halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa licha ya kulishukuru shirika hilo la Hand in Hand kwa masaada huo, amewataka wananchi waliopewa vifaa hivyo kuvitumia kama ilivyokusudiwa na kuwasisistiza wananchi wote  kuendelea kuchukua tahadhari ya UVIKO 19, kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na watalamu wa Afya, ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka, kuvaa barakoa wanapokuwa kwenye msongamano, kutumia vitakasa mikono na kupata lishe bora ili kuupa mwili kinga imara.

Aidha amewasisitiza wananchi wa halmashauri ya Arusha, hasa watu walio kwenye makundi yaliyo kwenye hatari zaidi na kuainishwa kupewa kipaumbele na serikali, wakiwemo Wahudumu wa afya, watu wenye magonjwa sugu, wenye umri wa kuanzia miaka 50 pamoja na walimu,  kwenda kupata chanjo ya UVIKO 19, chanjo inayotolewa kwenye Hospitali ya wilaya ya Olturumet, Hospitali ya Selian Ngaràmtoni, kituo cha afya Nduruma, zahanati ya Ngorbob iliyoko eneo la soko la Kisongo.

"Pamoja na kuchukua tahadhari za kujikinga na UVIKO 19, ni vema wananchi wakachoma chanjo, chanjo ambayo imethibitishwa na shirika la Afya Duniani,  na Serikali ya Tanzania kujiridhisha kupitia Wizara ya Afya, niwahimize wananchi, kuachana na maeneo ya uzushi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii, badala yake watafute taarifa sahihi kutoka kwa watalamu wa afya na si vinginevyo" amesisitiza Kaimu Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo, Kaimu mkurugenzi huyo, anawakaribisha wadau wa mashirika na watu binafsi wenye uwezo,  kujitokeza kusaidia halmashauri hiyo, kuwapa vifaa kwa ajili ya maeneo ya Umma yenye mikusanyiko ya watu, ikiwemo shule, masoko, standi lengo likiwa ni kuonheza nguvu za kupambana na maambukizi ya UVIKO 19, ugonjwa unaosababisha simanzi na uchungu kwenye jamii, zinazotokana na watu kupoteza wapendwa wao.

Awali shirika la Hand in Hand Eastern Africa Tz, limetoa jumla ya matanki  62 ya kunawia mikono kwenye mikusanyio, chupa 1,445 za sabuni za maji pamoja na  barakoa 1, 742, vifaa vitavyotumika kwenye  kwenye kata za Nduruma, Matevesi, Kisongo, Mwandeti, Laroi na Oljoro, zote zikiwa ni kata zilizoko maeneo ya pembezoni mwa halmashauri ya Arusha.


Kaimu







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.