Na. Elinipa Lupembe.
Shirika lisilo la kiserikali la Hand in Hand Eastern Africa (TZ), limetoa msaada wa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19, kwenye kata sita za pembezoni, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, maeneo ambayo shirika hilo linafanya kazi za kijamii na wananchi wa maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri ya Arusha, Mkurugenzi wa shirika hilo, Bi.Jane Sabuni, amesema kuwa shirika limefikia hatua hiyo, baada ya kushuhudia vifo vinavyotokana na UVIKO 19, ndani ya familia na jamii kwa ujumla, na kuona umuhimu wa uwepo wa vifaa vya kujikinga na UVIKO 19, kwa jamii zinazoishi maeneo ya vijijini, kutokana na ukweli kwamba kuna ugumu katika upatikanji vifaa kinha hivyo kutokana na umbali wa kufuata vifaa hivyo mijini.
Mkirugeznzi Jane amefafanua kuwa, shirika lao linafanya kazi ya kuwajengea uwezo wananchi juu ya ujasiriamali, hivyo ili wananchi hao wafikie malengo yaliyokusudiwa ni lazima wawe na afya bora, na ili kuwa na afya ni lazima kujikinga na UVIKO 19, kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tirirka pamoja na kuvaa barakoa wakati wa kufanya shughuli zao, hasa kwenye mikusanyiko ya watu wengi.
"Shirika linafanya kazi na wajasiriamali ambao wako kwenye risk kubwa ya kupata maabukizi ya UVIKO 19, kutokana na maeneo ya mikusanyiko wanayofanyia shughuli zao za kila siki, ili kuwaepusha kupata maambukizi, shirika limetoa matanki ya kunawaia mikono, sabuni za maji pamoja na barakoa, lengo likiwa ni kusaidia wadau wetu kujinga na UVIKO 19, waweze kufikiammalengo yao." Ameweka wazi Mkurugenzi Jane.
Naye Kaimu Mkurugenzi, Halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa licha ya kulishukuru shirika hilo la Hand in Hand kwa masaada huo, amewataka wananchi waliopewa vifaa hivyo kuvitumia kama ilivyokusudiwa na kuwasisistiza wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ya UVIKO 19, kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na watalamu wa Afya, ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka, kuvaa barakoa wanapokuwa kwenye msongamano, kutumia vitakasa mikono na kupata lishe bora ili kuupa mwili kinga imara.
Aidha amewasisitiza wananchi wa halmashauri ya Arusha, hasa watu walio kwenye makundi yaliyo kwenye hatari zaidi na kuainishwa kupewa kipaumbele na serikali, wakiwemo Wahudumu wa afya, watu wenye magonjwa sugu, wenye umri wa kuanzia miaka 50 pamoja na walimu, kwenda kupata chanjo ya UVIKO 19, chanjo inayotolewa kwenye Hospitali ya wilaya ya Olturumet, Hospitali ya Selian Ngaràmtoni, kituo cha afya Nduruma, zahanati ya Ngorbob iliyoko eneo la soko la Kisongo.
"Pamoja na kuchukua tahadhari za kujikinga na UVIKO 19, ni vema wananchi wakachoma chanjo, chanjo ambayo imethibitishwa na shirika la Afya Duniani, na Serikali ya Tanzania kujiridhisha kupitia Wizara ya Afya, niwahimize wananchi, kuachana na maeneo ya uzushi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii, badala yake watafute taarifa sahihi kutoka kwa watalamu wa afya na si vinginevyo" amesisitiza Kaimu Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo, Kaimu mkurugenzi huyo, anawakaribisha wadau wa mashirika na watu binafsi wenye uwezo, kujitokeza kusaidia halmashauri hiyo, kuwapa vifaa kwa ajili ya maeneo ya Umma yenye mikusanyiko ya watu, ikiwemo shule, masoko, standi lengo likiwa ni kuonheza nguvu za kupambana na maambukizi ya UVIKO 19, ugonjwa unaosababisha simanzi na uchungu kwenye jamii, zinazotokana na watu kupoteza wapendwa wao.
Awali shirika la Hand in Hand Eastern Africa (TZ), limetoa jumla ya matanki 62 ya kunawia mikono kwenye mikusanyio, chupa 1,445 za sabuni za maji pamoja na barakoa 1, 742, vifaa vitavyotumika kwenye kwenye kata za Nduruma, Matevesi, Kisongo, Mwandeti, Laroi na Oljoro, zote zikiwa ni kata zenye misongamano ya masoko na maeneo ya pembezoni mwa halmashauri ya Arusha.
Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa, akipokea barakoa kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la Hand in Hand Eastern Africa Tz, Bi. Jane Sabuni,( wapili kulia), wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kujinga na UVIKO 19, msaada uliotolewa na shirika hilo kwa kata sita za hamashauri ya Arusha.
Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa, akipokea chupa ya sabuni ya maji kwa ajili ya kunawia mikono, kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la Hand in Hand Eastern Africa Tz, Bi. Jane Sabuni,( wapili kulia), wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kujinga na UVIKO 19, msaada uliotolewa na shirika hilo kwa kata sita za hamashauri ya Arusha.
Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Arusha, mwalimu Hossein Mghewa, akinawa mikono mara baada ya kukabidhiwa msaada wa matanki ya kunawia mikono, na Mkurugenzi wa shirika la Hand in Hand Eastern Africa Tz, Bi. Jane Sabuni, vifaa kwa madhubuti vya kujinga dhidi ya maambukizi UVIKO 19, msaada uliotolewa na shirika hilo kwa kata sita za hamashauri ya Arusha.
Picha ya pamoja watumishi wa halamshauri ya Arusha na Watumishi wa shitika la Hand in Hand Eastern Africa Tz, mara baada ya makabidhiano ya Vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19, makabidhiano yaliyofanyika kwenye viwanja vya halamshauri yaArusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.