Na Elinipa Lupembe
Shirika la JICA kupitia mradi wake wa TANSHEP unaokwenda na usemi wa Anzia Sokoni, Malizia Shambani kwa kipato zaidi, limetoa mafunzo kwa wakulima namna ya kutafuta masoko ya mazao kwa njia ya mtandao.
Shirika hilo limetoa mafunzo ya jinsi ya kutafuta masoko ya mazao kwa njia ya mtando maarufu kama 'Anzia Sokoni App' teknolojia inayomuwezesha mkulima kuangalia bei za mazao kila siku kupitia simu yake ya kiganjani.
Mratibu wa Mradi TANSHEP Mkoa wa Arusha Naomi Buhama amesema kuwa, App hiyo imeunganishwa na masoko ya mazao nchi nziam hivyo inampa fursa mkulima kutafiti bei na uhitaji wa zao husika sokoni na kumsukuma kufanya uchaguzi wa zao la kulima kwa kuzingatia uhitaji wa soko kwa msimu husika.
Amesema kuwa Shirika limeboresha mfumo wa program ya Anzia Sokoni, malizia Shambani kwa kipato zaidi kwa kuwa ya kidigitali ambayo inamuwezesha mkulima kufanya utafiti wa maaoko ya mazao nchini kupitia simu yake ya kiganjani.
"Anzia Sokoni App, licha ya kuwawezesha wakulima kupata masoko nchini zaidi shirika huwaunganisha na watalamu wa kilimo chuo cha Tengeru kwa ajili ya mafunzo ya kilimo bora ili kuzalisha mazao bora ya kuingia kwenye ushindani wa soko" Amefafanua Naomi
Hata hivyo wakulima hao wamelishukuru shirika hilo kwa mafunzo hayo, ambayo wamethibitisha ni muhimu katika kufanya kilimo kinachoendana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia nchini.
Dina Mbise mkulima wa mazao ya mbogamboga Kijiji cha Sambasha, amebainisha umuhimu wa mafunzo hayo utakaowawesha wakulima kufanya tafiti za masoko na bei za mazao kupitia 'Anzia Sokoni App' mtandao ambao ni rahisi na unaokoa gharama na muda kwa mkulima kutafuta soko akiwa nyumbani.
"Zamani nililazimika kwenda sokoni kutafuta wateja wa mazoa yangu, kwa sasa wakulima tunatafuta soko kiganjani, na kuwa na uhakika wa soko nchi mzima na sio kutegemea soko kuu la hapa Arusha tuu, au madalali waliokuwa wakitunyonya wakulima". Amesema Dina.
Miraji mkulima wa kijiji cha Kiseriani amesema kuwa programu ya anzia sokoni imewatoa wakulima kwenye kilimo cha mazoe na kufikia kilimo biashara kutoka na mabadikiko ya kulima mazao yanayohitajika sokoni na sio kulima kwa mazoea.
"Kwa sasa tunalima mazao kwa kuzingatia uhitaji wa soko, hatulimi kwa kuongozwa na akili zetu, tunaongozwa na soko, "Anzia Sokoni App", itaongeza ufanisi mkubwa kwa wakulima pamoja na kupunguza gharama za utafutaji wa masoko wa kianalogia tulioufanya huko nyuma" Amesema Miraji.
Naye Afisa Kilimo Halmashauri ya Arusha Bahati Mtweve, amesema kuwa programu ya Anzia Sokoni imeanza kufanya mapinduzi makubwa kwa wakulima ambao sasa hulima kulingana na uhitaji wa mazao sokoni.
"Kupitia programu ya Anzia Sokoni malizia shambani kwa kipato zaidi, wakulima wameacha kilimo cha mazoea na kuingia kwenye kilimo biashara, kilimo ambacho ndio malengo ya serikali na utekelezaji wa Agenda 10- 30 ya Kilimo Biashara.
Awali halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika la JICA, wameendelea kuwasimamia wakulima kwa kuhakikisha wanalima kilimo cha kisasa kwa kuzingatia uhitaji wa zao ssokoni
"ARUSHA DC Ni Yetu, Tushiikiane Kuijenga"
#KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.