Na. Elinipa Lupembe.
Shirika la Ndoto in Action limekamilisha na kukabidhi mradi wa uboreshaji miundombinu ya shule ya msingi Marurani kata ya Nduruma halmsahuri ya Arusha, mradi uliogharimu shilingi milioni 118.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi huo, iliyofanyika shuleni hapo, mkurugenzi wa shirika la Ndoto in Action, Hussein Salim, amesema kuwa, shirika hilo linashirikiana na serikali katika kuboresha huduma za jamii nchini, katika sekta za elimu, afya na ustawi wa jamii shuleni, na kuongeza kuwa wamefanikiwa kuboresha miundo mbinu ya shule ya msingi Marurani pamoja na kuwajengea uwezo wanafunzi katika nyanja ya afya ya hedhi kwa wasichana.
Ameongeza kuwa ndoto in Action, imefanikiwa kujenga na kukabidhi jumla ya vyumba 4 vya madarasa, madawati 120, matundu 10 ya vyoo vya wasichana na sehemu ya kujihifadhi wakati wahedhi, mfumo wa kuvuna maji ya mvua wenye matenki 8 yenye uwezo wa kuhifadhi lita elfu 4 za maji, pamoja na miundombinu ya kunawia mikono.
"Shirika limewiwa kujenga choo cha wasichana chenye miundombinu ya maji na sehemu za kubadilishia taulo za kike kipindi cha hedhi lengo likiwa kuwoandolea wasichana changamoto ya kushindwa kuhudhuria masomo wakati wa hedhi, takwimu zinaonyesha zinaonesha, mtoto wa kike hushindwa kuhudhuria vipindi 3-4 kwa mwezi, vipindi 48 kwa mwaka wakati wa hedhi" ameweka wazi Mkurugenzi huyo wa Ndoto in Action.
Hata hivyo mkurugenzi Salim, amekubali ombi lililotolewa na uongozi wa shule hiyo ya Marurani la kukarabati vyumba vyote vya madarasa shuleni hapo, na kusema kuwa shirika linaanda mipango ya kutekeleza mradi huo wa kukarabati madarsa yote ya shule hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, licha ya kulishukuru shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita, amewataka walimu na wanafunzi kutumia miundombinu hiyo vizuri ili kuoandisha taaluma ya wanafunzi shuleni hapo.
"Tunaamini mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia yapo, kazi kwenu walimu na wanafunzi, kuongeza juhudi katika tendo la kujifunza na kufundisha ili lengo la serikali la kutoa elimu bora kwa wanafunzi wote litimie, wasichana mmewezeshwa kuwa na eneo la kujisitiri wakati wa hedhi, jambo ambalo litaongeza mahudhurio yenu shuleni, fanyeni jitihada katika masomo ili ufaulu wenu ulingane na mazingira bora mliyoandaliwa" amesisitiza Mkurugenzi Msumi.
Aidha Mkurugenzi Msumi, ameupongez mpango wa kujenga mfumo wa kuvuna maji ya mvuo, unaokwenda sambamba na miundombinu ya kunawia mikono, miundombinu itakayowawezesha jamii ya Marurani kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, ikiwa ni mpango wa maendeleo dhidi ya UVIKO 19.
Naye Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, mheshimwa Ojung'u Salekwa, ameushukuru hongozi wa shirika la Ndoto in Action na kusema kuwa mradi huo ni mkubwa na wa thamani katika sekta ya elimu ndani ya halmasahuri ya Arusha, na kuwataka kuendelea kutoa huduma hiyo kwa shule nyingine zenye mahitajimkama hayo.
Shule ya msingi Marurani ni miongoni mwa shule kongwe nchini ilianzishwa rasmi mwaka 1975, kutokana na kujengwa muda mrefu, miundombinu ya shule hiyo imekuwa chakavu, hivgo serilaki na wadau inaendela kuboresha miundombinu ya shuoe hiyo, mpaka sasa shule ina jumla ya wanafunzi 406, wasichana 210 na wavulana 196.
Arusha DC
KaziInaendeleaa✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.