Na Elinipa Lupembe
Shirika lisilo la kiserikali la SOS Children Village linalofanya shughuli zake ndani na nje ya halmashauri ya Arusha kupitia mradi wake wa Uimarishaji familia ulioanza kutekelezwa mwaka 2007 katika kata 11 umefanikiwa kuwezesha familia 514 kuimarika kiuchumi na kuweza kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto.
Aidha, mradi huo ambao umefikia tamati mwezi Disemba mwaka 2022 huku familia 346 zikiwa zimeweza kujitegemea kiuchumi ambapo ni sawa na asilimia 86 ya familia zilizokuwa zikinufaika na mradi huo
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha mradi huo iliyofanyika katika viwanja vya shirika hilo vilivyopo katika kata ya Oltrumet, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Arusha, Daniel Ngasikiwe amesema kuwa kuna kila sababu ya kulipongeza shirika hilo kwa kuwa kupitia mradi huo wamegusa maisha ya watanzania wengi hasa waliokuwa na hali ya uchumi duni.
“Tunatambua dhahiri kuwa endapo hakutakuwa na uchumi imara ndani ya familia inatoa mwanya wa vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto kufanyika katika familia husika, hivyo shirika la SOS kupitia mradi huu wamefanya jambo kubwa sana na la kipekee kwani familia hizi zinazohitimu leo zimeweza kujitegemea kiuchumi na tunaamini zitaenda kusaidia na familia zingine ambazo hazikubahatika kuwepo kwenye huu mradiKw
Kwa upande wake Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la SOS Children Village, Kaiza Sakafu, ameweka wazi kuwa wamekuwa wakifanya kazi na Jamii, familia na watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0-17 pamoja na vijana huku lengo kubwa likiwa ni kuwezesha familia na jamii kutoa ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kuwahudumia watoto na kuhakikisha wanaishi katika mazingiira mazuri na salama.
“Haikuwa kazi rahisi, tunaamini kile ambacho tumeweza kuwasaidia watakithamini na kukitunza na hatimaye waweze kuizisaidia na familia zingine zinazowazunguka”. Amesisitiza Sakafu huku akitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau kuendelea kutoa ushirikiano ili miradi mingie kama hiyo iweze kuifikia jamii nyingi zaidi na kuleta mafaniHata
Hata hivyo wanufaika wa Mradi huo wameonekana kujawa na furaha tele wakati wa hafla hiyo fupi ya kuhitimu na kulishukuru shirika hilo pamoja na wadau walioshirikiana na kusema kuwa mradi huo umekuwa na manufaa makubwa sana kwao kwani sasa wanaweza kujitegemea kwa kiasi kikubwa na kutoa malezi bora kwa familia Kabl
“Kabla ya kukutana na SOS, nilikuwa mama wa nyumbani nikiwa siwezi kujikimu na kitu chochote lakini baada ya kujiunga na mradi huu mwaka 2020 sasa ninaweza kujikimu kimaisha mimi pamoja na familia yangu kwa kuwa sasa ninajua kushona nguo za mitindo mbalimbali na tuna kikundi cha akina mama.” Alisema Zulfa Athuman ambaye ni mama wa watoto wawili kutoka kata ya Oloirien alipozungumza mara baada ya hafla hiyo kuahirishwa.
Awali, Shirika hilo linatekeleza miradi mingine ya kijamii kwa kuendelea kupanua wigo zaidi wa kuzifikia jamii nyingi katika maeneo tofauti tofauti katika Mkoa wa Arusha huku likijikita kufanya kazi na familia, watoto na jamii kwa ujumla.
ARUSHA DC
KaziInaendelea ✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.