Na. Elinipa Lupembe.
Shirika la Tumaini Jipya -New Hope Tanzania, limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto na kuepusha ndoa na mimba za utotoni kwa kujenga bweni la kulala wasichana 80, shule ya sekondari Lengiave, kwa gharama ya shilingi milioni 100.6.
Akizungumza wakati alipotembekea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bweni hilo, mkurugenzi wa shirika la Tumaini Jipya Louise Richardson, amesema kuwa, shirika lao limefikia uamuzi wa kujenga bweni la wasichana, kwa lengo la kuwawezesha wasichana wa Lengijave, kupata muda wa kujisomea na kutimiza ndoto zao, ndoto ambazo wasichana wengi walilazimika kuzikatiza, kutokana na ndoa na mimba za utotoni, zilizotokana na mila na desturi za jamii ya kimaasai.
Louise ambaye ni raia wa Uingereza, aliyewahi kuishi kijiji cha Lengiajve kama 'volunteer' ameweka wazi kuwa, kipindi alichoishi Lengijave, alijionea namna wasichana wanashindwa kufikia malengo na ndoto zao, kutokana na kukosa fursa ya kusoma na kukamilisha safari ya masomo yao, kutokana na mila lakini pia kukosa fursa za kujiendeleza kimasomo.
"Nimeishi Lengijave, nawapenda sana wananchi wa Lengijave, ni rafiki zangu, ninatambua changamoto zinazowakabili wanachi wa Lengijave hasa wanawake na wasichana, hivyo tumeona ni bema kutafuta mbinu za kuwawezesha watoto wa kike, kujikwamua kifkra, kwa kusoma katika mzazingira bora" ameweka wazi Louise.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amelishukuru shirika la Tumaini Jipya kupitia mkurugenzi wake mama Louise, na kuweka wazi kuwa, halmashauri inathamani mchango wa ASAS hiyo, hasa kwa kutataua changamoto zinazowakabili watoto wa kike wanaotokea katika jamii za kifugaji, na kuahidi kuendela kushirikiana na shirika hilo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na ustawi wa jamii ya kitanzania.
Hata hivyo wanafunzi wa shule ya sekondari Lengijave, wamefurahishwa na uwepo wa bweni hilo la wasichana na kusema kuwa, bweni hilo litawawezesha wasichana kusoma kwa utulivu na kukabiliana na changamoto za ndoa na mimba za utotoni zilizokuwa zinawkabili wasichana wengi wa Lengijave.
Dayana Frank mwanafunzi wa kidato cha III, amesema kuwa ameona tofauti kubwa ya kusoma akiwa bweni na akiwa nyumbani, kwa kuwa licha ya kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni lakini pia mazingira ya nyumbani hayamuwezeshi mtoto wa kike kujisomea kutokana na kupangiwa kazi nyingi za nyumbani mara baada ya kutoka shuleni.
Naye mkuu wa shule ya sekondari Lengijave, mwalimu Sunday Joseph, amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo adhimu, msaada ambao unategemewa kuleta mabadiliko chanya shuleni hapo, kwa kuongeza kasi ya ufaulu kwa wasichana pamoja na kupandisha taaluma ya shule.
"Mara nyingi, licha ya umbali mrefu anaotembea mwanafunzi kwenda na kurudi shuleni, lakini bado watoto wa kike hawapati nafasi ya kujisomea wawapo nyumbani, kutokana na kutumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani, lakini pia wanakuwa kwenye hatari ya kukatishwa masomo, kutokana na mazingira na mila na desturi, uwepo wa bweni, utawafanya kutulia na kuelekeza mawazo yao katika masomo, tofauti na kuishi nyumbani" amesisitiza mkuu huyo wa shule.
Mkuu huyo wa shule amesema kuwa, tayari bweni hilo limeanza kutumika kama kambi, kwa wasichana wa kidato cha nne, wanaoendelea na mtihani wao wa Taifa kidato cha IV, 2021.
Awali shule ya sekondari ya Lengijave, ina jumla ya wanafunzi 387, wasichana 240 na wavulana 147, huku karibu asilimia 30 ya wanafunzi wa shule, wakikadiriwa kutembe umabali wa takribari Kilomita 10 mpaka 15 kwenda na kurudi shuleni.
#TUMAINI JIPYA - NEW HOPE - KaziInaendelaa..✍✍✍
#ARUSHA DC - KaziInaendelea...✍✍✍
#LENGIJAVE - KaziInaendela....✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.