Na. Elinipa Lupembe.
Shirika la kimataifa la WaterAid Tanzania kwa kushirikiana na halmashauri ya Arusha, wamekamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya tabia chanya za Afya, kwenye shule nane za msingi katika halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule amethibitisha kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo, kwa shule nane za msingi, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 105, kufuatia fedha za ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya nchini Uingereza - DFID na kutekelezwa na shirika la WaterAid Tanzania.Licha ya kuwashukuru wafadhili wa mradi huo,.
Mkurugenzi Mtambule, ameweka wazi kuwa, mradi huo umefanyika wakati muafaka, kutokana na ukweli kwamba shule za serikali katika halmashauri hiyo, zinao uhitaji mkubwa wa miundombinu bora ya vyoo na sehemu za kunawia mikono, kutokana na ongezeko la idadi kubwa ya wanafunzi, wanoandikishwa katika shule hizo tangu utekelezaji wa elimu bila malipo ya mwaka 2015, na kuanza raami mwaka 2016.
Ameongeza kuwa, uwepo wa miundombinu bora ya kunawia mikono shuleni, utawajengea uwezo wanafunzi kufahamu umuhimu wa kunawa mikono kwa nyakati tano muhimu pamoja na kuwa na tabia chanya za afya katika umri mdogo pamoja na kuwawezesha kujikinga na magonjwa yanayotokana na uchafu unaoshikwa kwa mikono.
Naye Mratibu wa Mradi WaterAid Arusha na Manyara, Upendo Muntambo, amesema kuwa mradi huo wenye lengo la kuwafanya wanafunzi kuwa na tabia chanya za afya za kunawa mikono kwa nyakati zote muhimu, zaidi mara wanapotoka chooni huku wakiendelea kuchukua tahadhari ya magonjwa ya kuhara, homa za matumbo, kipindipindu pamoaja na gonjwa hatari la Corona.
"Shirika la WaterAid kwa ufadhili wa DFID, limeona kuna umuhimu wa kuboresha miundombinu ya vyoo na sehemu za kunawia mikono kwenye shule za msingi, lengo likiwa ni kuwajengea wanafunzi tabia ya kunawa mikono mara kwa mara ili kujikinga na maradhi yanayotokana na uchafu wanaoushika kwa mikaono yao" amesema Mratibu huyoNao
Nao wajumbe wa Kamati za shule hizo nane, wamelishukuru shirika la WaterAid kwa kuona umuhimu wa kuboresha vyoo na miundombinu ya maji shuleni, kwani tatizo lilikuwa ni kubwa na lina hatarisha afya za watoto wao wawapo shuleni.Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya Msingi Olosiva, Stevene Songoyo, amesema kuwa uwepo wa vyoo bora vyenye miundo mbinu bora ya kunawia mikono shuleni, utawakinga wanafunzi kupata magonjwa yanayotokana na uchafu ikiwemo homa za matumbo, kuharisha pamoja na gonjwa hatari la Corona.
Hata hivyo Afisa Afya, halmashauri ya Arusha, Issa Msumari amesema kuwa, ujenzi wa miundombinu hiyo,umeambatana na utoaji elimu na uanzishwaji wa klabu za usafi katika shule hizo, klabu ambazo zitasimamia utunzaji wa miundimbinu pamoja na wanafunzi hao kuelemishana juu ya umuhimu wa unawaji mikono mara baada ya kutoka chooni sambamba na kufuatilia mwenendo wa matumizi ya miundombinu hiyo kwa usimamizi wa walimu wa Afya katial shule hizo.
Aidha utekelezaji wa mradi huo, umehusisha ukarabati wa vyoo na miundombinu ya maji, ujenzi wa sehemu za kunawia mikono, kampeni ya kuhamasisha tabia chanya za afya pamoja nanuanzishwaji wa Klabu za Afya kwenye shule zote zilizopata mradi huo, ikiwa ni pamoja na shule ya msingi Olosiva, Mringa, Seliani, Olmotonyi, Lemanyata, Leminyoro, Oldonyosambu na shule mpya ya Enaboishu Academy.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.