Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Dkt. Ojung'u P. Salekwa, awataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa taarifa za matukio ya ukatili yanayoendelea katika jamii na akasema kwamba kutotoa taarifa ya matukio ya ukatilii kunatoa mwanya kwa vitendo hivyo kuendelea.
Aidha, alibainisha kuwa kuelekea siku 16 za kupinga ukatilii, Halmashauri inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa elimu kuhusu madhara ya ukatili na njia za kuzuia zinawafikia watu wote, hasa wale wanaoishi vijijini ambako mara nyingi matukio ya ukatili hufichwa.
Alihitimisha kwa kuwahamasisha wananchi kushirikiana kwa karibu na viongozi wa mitaa, mashirika ya kijamii, na vyombo vya usalama katika kukomesha ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.