• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SNV YAWEZESHA KATA 14 ARUSHA DC, KUFIKIA ASILIMIA 95% YA KAYA KUWA NA VYOO BORA.

Posted on: March 14th, 2020

Na. Elinipa Lupembe.

Shirika lisilo la kiserikali la SNV, limemaliza muda wake, kupitia mradi wake wa Ujenzi wa Vyoo Bora, huku likiwa limepata mafanikio makubwa ya  kuweziwesha kata 14 za halmasuri ya Arusha kufikia asilimia 95% ya kaya kuwa na Vyoo Bora,

Akizungumza kwenye kikao maalumu cha kufunga mradi na kuaga, kikichofanyika kwenye ukumbi wa Mwenyekiti, halmashauri ya Arusha,, Meneja wa shirika la SNV Tanzania, Jackson Wandera, amethibitisha kumalizika kwa muda wa utekelezaji wa mradi huo, kwa mafanikio makubwa, yaliyowezesha kata 14 kufikia asilimia 95 ya kaya kuwa na vyoo bora, kutoka asilimia... walioikuta mwaka 2017 walipoanza mradi huo.


Amefafanua kazi zilizozitekeleza katika mradi huo ni pamoja na kuhamasisha  na kutoe elimu ya ujenzi wa vyoo bora kwenye kaya, kuhamasisha tabia chanya za afya za kunawa mikono nyakati tano muhimu, pamoja na kutoa elimu ya afya shule kwa kuunda Klabu za afya shuleni.

"Tumepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha asilimia 95 ya kaya kwenye kata 14 za halmashauri ya Arusha,kujenga vyoo bora vyenye sehemu ya kunawia mikono, pamoja na kuhamasisha unawaji mikono nyakati tano muhimu" amesema Wandera.

Hata hivyo,  Wandera ameweka wazi kuwa, licha ya mafanikio hayo ya  kufikia asilimia 95 ya kaya kuwa na vyoo bora, bado jamii inakabiliwa na changamoto ya unawaji mikono nyakati tano muhimu kwa kuwa mradi umefanikiwa kufikia asilimia 5 tu, na kuitaka halmashauri kuendeleza kampeni hiyo ya unawaji mikono kwa kuwa tayari watalamu wamekwishajengewa uwezo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Baraka Simoni, amelishukuru na kulipongeza shirika la SNV, kwa ushirikiano na kazi nzuri iliyoifanywa kwa wananchi wa halmashauri ya Arusha, kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo, na kuahidi kuendelea kusimamia mradi huo ili uwe endelevu kwa manufaa ya afya za wananchi wa halmashauri hiyo.

Aidha Mwenyekiti huyo, amewataka watalamu wa halmashauri, kuendelea kutoa elimu kwa jamii ya matumizi sahihi ya vyoo hivyo kwenye kaya, sambamba na kuongeza nguvu katika kampeni ya tabia chanya ya kunawa mikono kwa maji na sabuni, nyakati tano muhimu.

"Kunawa mikono ni jambo linalofanywa na mtu mwenyewe binafsi, niwatake wananchi kubadili tabia na kuanza kunawa mikono kwa maji na sabuni, katika nyakati tano muhimu" amesisitiza Mwenyekiti huyo.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii, Angela Mvaa, kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, halmashauri ya Arusha,  amesema kuwa, halmashauri ina imeweka mikakati ya kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya vyoo bora na unawaji mikono kwa sababuni na kuhakikisha jamii nzima inakuwa na tabia chanya za kiafya.

Aidha Angela, amekiri kuwa, kupitia mradi wa SNV na kampeni ya kitaifa ya Nyumba ni Choo, halmashauri imeweza kufikia asilimia 99 ya kaya zenye vyoo, huku asilimia 75 vyoo bora, asilimia 24 vyoo duni, huku ikibakiza asilimia 1 tu na kuitaka jamii kuendelea kujenga nyumba zenye vyoo bora.

Shirika la SNV, limetekeleza mradi wa Ujenzi wa Vyoo Bora na unawaji mikono kwa sabuni kwa sabuni kwenye kata 14, vijiji 36 na vitongoji, kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia Februari 2017 mpaka Februari 2020.









Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.