Hayawi hayawi yamekuwa, hatimaye serikali ya kijiji cha Samaria kata ya Nduruma imefanikiwa kuanzisha soko jipya la kila siku la bidhaa za chakula ndoto ambayo waliisubiri kwa zaidi ya miaka 20.
Soko hilo limekuja kufuatia mpango wa serikali wa kuandaa maeneo rasmi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo kufanyia biashara zao na kundoka kwenye maeneo yasiyo rasmi ambayo ni hatarishi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa amekata utepe sokoni hapo, ishara yauzinduzi wa soko hilo na kuahidi kuendelea kulifanyia maboresho soko hilo, na kuwasihi wafanyabiashara kutambua kwa kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha
Hata hivyo wafanyabiashara wote wanatakiwa kuondoka kwenye maeneo yasiyo rasmi na kuhamia kwenye soko hilo rasmi.
Arusha DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.