Somo la Shule Salama na ulinzi na usalama wa mtoto kuanzia nyumbani mpaka shuleni limewaingia Wazazi wa kijiii cha Olmapinu, kata ya Bwawani, mara baada ya kupewa somo hilo na wataalamu wa halmashauri ya Arusha wakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya awali shule ya msingi Olokii.
Wazazi hao wamekiri somo hilo limewaingia vema na kuwafumbua macho, mara baada ya kupata semina fupi kupitia programu ya Shule Salama inayosisitiza wazazi, walezi na jamii kushirikiana na walimu kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto unanzia nyumbani, awapo njiani mpaka kufika shule, mtoto huyu anatakiwa kulindwa dhidi ya ukatili wa aina yoyote ile.
Lazaro Loserian amekiri kuona umuhimu wa wazazi na jamii nzima kushirikiana kumlinda mtoto, kutokana na ukweli kwamba, kulingana na ukubwa wa kijiji chao, mtoto hutembea maeneo hatarishi kutoka nyumbani mpaka kufika shuleni, jambo ambalo jamii inalo jukumu la kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto.
"Maeneo yetu yana mashamba makubwa, hata mzazi ukimlinda mtoto nyumbani na mwalimu akamlinda shuleni bado kuna changamoto ya usalama wa mtoto akiwa njiani kuelekea shule ama kurudi nyumba, ni vema jamii nzima tuungane kuahikisha usalama wa watoto wetu katika maeneo yote" Amesema Loserian
Naye Rashi Hassan amekiri kuwa licha ya kumpa mtoto mahitaji yake muhimu ya shule bado kunahitajika nguvu ya kumlinda mtoto dhidi ya ukatili.
"Somo hili limetupa uelewa mkubwa juu ya Usalama wa Mtoto, licha ya kuwapa watoto mahitaji yote lakini tusipomlinda ni kazi bure, tutaungana kuwalinda watoto watimize ndoto zao, tunahitaji wasomi na watalamu kutoka kijijini kwetu Olmapinuu" Amesisitiza Hassan
Ndikonyi Ndaya amefafanua kuwa, Serikali inatekeleza jukumu lake la kujenga shule na madarasa mazuri, lengo likiwa watoto wapate elimu na kupata watalamu wa fani mbalimbali, ili kufikia lengo la serikali wazazi na jamii tunalo jukumu la kuhakikisha Shule Salama kwa kuwalinda watoto wote dhidi ya ukatili.
"Shule yetu haina bweni, kama wazazi na walezi tutahakikisha mtoto huyu analindwa, progam ya shule salama imetufungua macho, tutahakikisha majengo haya ya shule yanatoa watalamu kwa kuhakikidha usalama wa mtoto" Amesisitiza Ndaya
Watalamu wa halmashauri kupitia wanatoa elimu kwa jamii juu ya ulinzi na usalama wa mtoto kupitia programu ya Shule Salama inayotekelezwa kupitia miradi ya ujenzi wa shule za awali na miradi ya GPE- LANES II.
Kumbukwe kuwa imetoa fedha kiasi cha shilingi Milioni 115.6 kwa awamu mbili kupitia miradi ya GPE - LANES II kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule mbili za Msingi za Msingi Ngorbob kata ya Matevesi na shule ya Msingi Olokii kata ya Bwawani.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.