Na Elinipa Lupembe
Shirika la SOS Tanzania kwa kushirikiana na Meta Sport limeanza mchakato wa maandalizi ya mbio za Ngorongoro Race Marathon ili kupata fedha za kuwahudumia watoto wenye mahitaji na waishio kwenye mazingira magumu mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha, Meneja wa Mradi mkoa wa Arusha, Noa Mwakaragwa amesema kuwa, mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba 2023 wilaya ya Karatu, zikiwa na lengo la kukusanya shilingi milioni 160 kwa ajili ya kuwahudumia watoto waishio kwenye mazingira hatarishi.
Amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, hivyo shirika limewiwa kushirikiana na wadau wengine kutafuta fedha za kukabiliana na changamoto zinazowakabili watoto na ikiwezekana kudhibiti tatizo hilo lisiendelee kutokea.
"Shirika la SOS linajihusisha na malezi ya watoto ya kifamilia kupita vituo vyake vya watoto nchini, kwa kutambua umuhimu wa mtoto kuishi kwenye familia, kupitia fedha zitakazopatikana, shirika limeandaa mifumo itakayohakikisha watoto hawaingi tena mitaani bali wanalelewe kwenye familia, kupitia walezi wa kuaminika ili wapate malezi bora na kuweza kuzifikia ndoto zao kama ilivyo watoto wengine" Ameweka wazi Mwakaragwa
Naye Mkurugenzi wa fund raising Emmanuel Sanga, ameweka wazi utaratibu wa mbio hizo Mbio zenye ubora mkubwa ambapo kila mshirikia atajisajili kwa shilingi elfu 35 na zitajumuisha mbio za
Km 21, Km 10 na Km 5 huku Km 2.5 zitakuwa kwa ajili ya watoto, na watajisajili bila malipo.
"Tunawakaribisha watu wote kushiriki Mbio hizi, zitakazofanyika Karatu na tunategemea kushiriki zaidi ya watu elfu tatu, ikiwemo watu binafsi, mashirika ya umma, dini, binafsi, taasisi pamoja na makampuni lengo likiwa ni kupata fedha kwa ajili ya uendeshaji wa program za maalezi ya watoto waishio kwenye mazingira hatarishi wilaya ya Karatu" Amebainisha Sanga.
Naye Katibu wa chama cha Riadha mkoa wa Arusha, Rogan Steven licha ya kulipongeza shirika la SOS kwa kugusa jamii kupitia mchezo wa riadha, ameahidi chama hicho kutoa ushirikiano kwa kuhamsisha wanariadha kushiriki kwa wingi pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi mbio hizo zinazogusa jamii moja kwa moja.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.