Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, anautaarifu Umma kuwa Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 527.9 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu katika sekta ya Afya, Elimu na Umwagiliaji.
Mkurugenzi Msumi amefafanua kuwa jumla ya shilingi milioni 357.05 zitatumika kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Bwawani zikijumuisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la Wazazi (martenity ward) na ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Afya yenye sehemu mbili (2 in 1). Ameitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa uzio wa shule ya sekondari Oldonyowas utakaogharimu shilingi milioni 79.5 pamoja na ukarabati wa mfereji wa Umwagiliaji Timbolo utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 91.4.
Aidha miradi hiyo itatekelezwa kwa kuzingatia taratibu na matumizi ya ’force Akaunti’ kwa muda wa miezi 12, huku shughuli za utekelezaji wa miradi hiyo, zikifanyika kwenye ngazi ya jamii kwa Usimamizi na Ushauri wa kitalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.