Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, anawatangazia wananchi wote, kuwa Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani, wa robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2021/2022, utafanyika tarehe 14.02.2022 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:00 asubuhi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa, wenye lengo la kujadili taarifa za utekekezaji wa shughuli za Maendeleo zilizotekelezwa kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022, kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba - Desemba 2021.
Aidha Mkutano huo utakuwa na agenda 10, agenda kuu zikiwa ni Maswali ya Papo kwa papo, Taarifa za Utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili cha kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2021, Taarifa ya Mapato na Matumizi kwa mwezi Desemba 2021, pamoja na kupitisha Mihtasari ya Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Arusha za taarifa za robo ya pili.
Mkutano huo ni wa wazi, hivyo wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria mkutano huo.
ARUSHA DC
# KaziInaendelea✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.