TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Watanzania kukemea vitendo vya ukatili ulioshamiri dhidi ya wanawake na watoto na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa dhidi ya wahusika.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Magharibi lililofanyika katika Ukumbi wa NSSF mkoani Kigoma. Ametaja baadhi ya vitendo hivyo kama mauaji, ubakaji, ulawiti, kupigwa, kunyanyaswa, kunyimwa haki za kumiliki ardhi na mali nyingine za familia, urithi, fursa za elimu, ukeketaji, adhabu kubwa zisizowiana na kosa alilotenda mtoto.
Makamu wa Rais amesema baadhi ya vitendo hivyo vinafanywa na wanafamilia au ndugu wa karibu na sehemu kubwa ya vitendo hivyo havitolewi taarifa kwenye vyombo vya sheria ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. Ameongeza kwamba wakati mwingine, baadhi ya mila na desturi katika jamii hutumika kuwakandamiza wanawake na watoto.
Aidha Makamu wa Rais ametoa rai kwa Kongamano hilo ambalo idadi kubwa ya washiriki wake ni wanawake na ambao ni walezi wa familia, kuelekeza nguvu pia katika kumlinda mtoto wa kiume ili kumhakikishia usalama wake. Amesema uwekezaji jitihada kidogo kwa mtoto wa kiume imepelekea mtoto wa kiume kujikuta katikati ya matatizo lukuki yakiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, ushoga na aina nyingine za ukatili.
Makamu wa Rais ili kuendelea kuongeza mchango na ushiriki wa Wanawake katika utunzaji wa mazingira na kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia, hakuna budi kongamano hilo kujadili na kuibua mikakati madhubuti na yenye kutekelezeka ili kufikia malengo hayo.
Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha utoaji wa elimu na hamasa kwa umma kuhusu utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi ya kupikia. Amesema elimu kwa umma na hamasa ni muhimu katika utunzaji endelevu wa mazingira kwa kuwa tabiawatu ndiyo kisababishi kikuu cha uharibifu wa mazingira
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.