Na Elinipa Lupembe.
Diwani wa viti Maalum Mhe. Grace Seneu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata ya Bwawani kwa kipindi ya robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 ya kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2023.
Akiwasilisha taarifa hiyo Mhe. Grace ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongwa na mama Samia kwa kuwapa fedha nyingi zilizotekeleza miradi ya maendeleo kwa awamu hiyo ikiwemo shilingi milioni 81.3 za ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa, kupitia miradi ya BOOST, milioni 350 kujenga kituo cha afya kupitia fedha za TASAF, shilingi milioni 57.8 za ujenzi wa darasa la awali kupitia fedha za mradi wa GPE - LANES II.
Licha ya mafanikio mengi Mhe. Grace amezitaja changamoto zinazoikabili kata hiyo ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara na madaraja unaotakana mvua za masika, na kumuomba mkurugenzi wa halmashauri kupeleka mitambo ili kunusuru tatizo hilo la barabara wakati wakisubiri TARURA kufanyia kazi barabara hizo.
Aidha amezungumza kwa masikitiko makubwa juu ya ukosefu wa nyumba za walimu kwa shule za msingi na sekondari, unaosababaisha watumishi hasa walimu kushindwa kuishi Bwawani kutokana na ukosefu huo wa nyumba.
"Tunafahamu mazingira ya Bwawani na magumu ni vema serikali kuweka kipaumbele kwa kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za watumishi hususani walimu ili wawezesha watymishi kukaa Bwawani, hali ngumu inawafanya walimu kutafuta uhamisho pind8 wanaponagiwa kufanya kazi pale."Amesema Mhe. Grace
Hata hivyo Mhe. Grace ameishukru serikali kupitia REA kwa kuweka umeme kwenye vijiji vya Bwawani na kuomba kuendelea kukamilisha kwenye vitongoji ambavyo bado havijapata umeme na kuongeza kuwa wananchi wa Bwawani wanapenda maendeleo hivyo uwepo wa umeme, utaharakisha maendeleo ya wananchi wa kata hizo.
Mkutano huo umefanyika kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.