Na Elinipa Lupembe
Diwani wa Kata ya Kisongo Mhe. Godson Lining'o akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata ya Oldonyosmabu kwa kipindi ya robo ya nne ya kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2023.
Mhe. Loning'o ameishukuru serikali kwa kujenga zahanati mbili za Ilkerini na LoovLukuny pamoja na kuwaunga mkono wananchi wa kata ya Kisongo katika ujenzi wa vyoo vya zahanati na kwasasa inatoa huduma vizuri.
Hata hivyo Mhe. Loning'o amezitaja changamoto zinazoikabili kata hiyo ni pamoja na nyumba ya daktari katika zahanati ya kijiji Cha Engorola na ukosefu wa maji katika Kijiji hicho pamjo na ukosefu wa umeme wa REA.
Aidha Mhe. Loning'o amemaliza kwa kuiomba serikali kupeleka maji na umeme kwenye baadhi ya vijiji na vitongoji vya kata hiyo pamoja na kukarabatia nyumba za madaktari kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwenye zahanati ya Engorora.
"Serikali ya awamu ya sita inafanya kazi nzuri ya kutekelza miradi inayotoa huduma kwa wananchi wetu, lakini wananchi wa Kisongo wanaiomba serikali kuwaondolea kero ya ukosefu wa nishati ya Umeme, mradi unaotekelzwa na REA kwa kuwa kuna baadhi ya vitongoji kwenye baadhi ya vijiji havijapata umeme huo" Amesisitiza Mhe. Diwani
Mkutano huo umefanyika kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.