Diwani wa viti Maalum Mhe. Nina Masanja akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata ya Kiutu kwa kipindi ya robo ya nne ya kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2023.
Akiwasilisha taarifa hiyo Mhe. Nina ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa niaba ya wananchi wa Kiutu kwa serikali kujenga shule ya sekondari ya kata kupitia mradi wa SEQUIP
Ameweka waai kuwa shule yao ya sekondari Kiutu, ambayo tayari wanafunzi wameanza masomo kwa mwaka wa masomo ulioanza Januari 2023, imewapunguzia wanafunzi kwenda kusoma shule za jirani pamoja na kuwafanya wananchi wa Kiutu kujisikia kuwa serikali yao inawajali sawa na watanzania wengine.
Aidha ameishukuru serikali kwa kuwajengea kipande cha barabara ya Kilimakikali na kuiomba serikali kukamilisha ujenzi wa barabara yote ili kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi wa kata ya Kiutu
Mkutano huo umefanyika kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.