• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TAKUKURU RAFIKI YAZINDULIWA RASMI HALMASHAURI YA ARUSHA

Posted on: January 24th, 2023

Programu mpya ya TAKUKURU RAFIKI ambayo inalenga kuwashirikisha zaidi wadau na Taasisi mbalimbali katika kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa hasa katika utoaji na upokeaji wa huduma za kijamii pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo imezinduliwa rasmi katika halmashauri ya Arusha kama sehemu ya msingi wa kukuza ustawi wa Utawala Bora.


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Arumeru Deo Mtui, amezindua programu hiyo mbele ya Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Arusha wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.


Uzinduzi huo umekuja kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo itaongeza wigo wa ushirikishwaji wa wananchi na wadau mbalimbali kutambua na kutatua kero katika utoaji wa huduma za kijamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, programu ambayo itadumu kwa muda wa miaka 4.


Aidha, Mtui amebainisha kuwa ngazi za Kata ni sehemu ya awali ya kutambua utatuzi wa kero zinazoweza kusababisha uwepo wa vitendo vya rushwa kwenye utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya maji, Elimu, Nishati, Afya, Barabara pamoja na Ardhi.


“Kupitia vikao tutakavyofanya na wananchi pamoja na wadau mbalimbali tutaweza kubaini na kutambua kero zinazoweza kusababisha kutokea kvi vitendo vya rushwa na kushirikiana kupanga mikakati ya kuzitatua mapema, hivyo ni wajibu wetu waheshimiwa madiwani Kwenda kusimamia na kupata mrejesho wa majawabu ya kero zilizoibuliwa kwenye vikao ili vitendo vya rushwa viweze kupungua katika Kata zetu”. Amesisitiza Mtui.


Hata hivyo waheshimiwa madiwani ambao ndio wamepewa jukumu la kuongoza vikao hivyo katika Kata, wamekiri kuipokea programu hiyo na Kwenda kuifanyia kazi huku wakikiri kuwa uwepo wa kero zinazodumu kwa muda mrefu ndani ya jamii kunapelekea vitendo vya rushwa kufanyika hivyo ujio wa programu hiyo kutaboresha uwazi na uwajibikaji katika kata zao sambamba na haki kutendeka ipasavyo.

“Tunamshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta wazo hili la ushirikishwaji wa wananchi na wadau mbalimbali katika kutokomeza vitendo vya rushwa, hili ni jukumu kubwa ambalo tumepewa sisi Madiwani na tutaenda kutekeleza hasa kwa kutoa elimu sehemu mbalimbli ili kuijenga nchi yetu”. Amesema Mhe. Justine Lendatai, Diwani wa Kata ya Bwani.

Awali, program hiyo itaenda kuimarisha utoaji wa huduma katika ngazi ya Kata, kuboresha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, uwajibikaji wa pamoja, kuimarisha uzingatiaji wa misingi ya Utawala Bora na kupunguza vitendo vya rushwa ndani ya halmashauri.


ARUSHA DC NI YETU

TUSHIRIKIANE KUIJENGA✍✍


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Arumeru Deo Mtui, akizundua TAKUKURU RAFIKI mbele ya Waheshimiwa Madiwani halmashauri ya Arusha.


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Arumeru Deo Mtui, akimkabidhi Mhe. Baraka Simon aliyeongoza Mkutano wa Baraza la madiwani kabrasha lenye mwongozo wa TAKUKURU RAFIKI wakati wa mkutano Maalum  wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha.


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Arumeru Deo Mtui, akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi na Mkuu wa kitengo cha Sheria Monica Mwailolo kabrasha lenye mwongozo wa TAKUKURU RAFIKI wakati wa mkutano Maalum  wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha.


Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, halmasahuri ya Arusha.


Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, halmasahuri ya Arusha.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI WA NAFASI ZA UDEREVA TAREHE 28/12/2018 December 19, 2018
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI TAREHE 1-7, AGOSTI 2020. July 31, 2020
  • TANGAZO KWA WANANCHI WOTE MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI 2O20/2021 TAREHE 29.01.2021 January 29, 2021
  • KINGA TIBA YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO KWA WATOTO MIAKA 5-14 March 02, 2021
  • Tazama zote

Habari mpya

  • BALOZI WA JAPAN NCHINI AMEKABIDHI MTAMBO WA KICHUJIA MAJI KUONDOA MADINI YA FLORAIDE KIJIJI CHA LEMANDA

    January 28, 2023
  • BALOZI WA JAPAN NCHINI AMEKABIDHI MTAMBO WA KICHUJIA MAJI KUONDOA MADINI YA FLORAIDE KIJIJI CHA LEMANDA

    January 28, 2023
  • MWENYEKITI ARUSHA DC MHE. OJUNG'U SALEKWA AKIPANDA MTI ENEO LA MTAMBO WA KUCHUJIA MAJINKIJIJI CHA LEMANDA

    January 27, 2023
  • BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA AZINDUA MTAMBO WA KUCHUJIA MAJI KIJIJI CHA LEMANDA....

    January 27, 2023
  • Tazama zote

Video

MFUGAJI AKIELEZEA FAIDA ZA UHIMILISHAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA - BANDA LA MIFUGO ARUSHA DC
Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.