Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi anawatangazia wafanyabiashara wote kuwa kutakuwa na zoezi la kukusanya madeni kwa wafanyabiashara ambao hawajalipia kodi na ada za biashara zao kama ifuatavyo: -
1. Leseni za biashara
2. Leseni za Vileo
3. Ushuru wa Nyumba za kulala Wageni (Hotel Leavy)
4. Kodi ya Huduma (Service Leavy)
Adhabu kwa wakwepaji wa ushuru/ada mbalimbali za halmashauri Pamoja na masharti yake.
Zoezi hilo litafanyika kwa kushirikiana na Wakala wa Kampuni ya Receivable's Solutions Co. Limited. kwa Mkataba Na. LGA/007/2022/23/HQ/NC/01 Lot 13 wa kukusanya madeni ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na adhabu ya kukiuka masharti ya Leseni.
Kulingana na sheria, sura ya 208 kifungu cha 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake ya mwaka 2002, kila mfanyabiashara anatakiwa kulipia ada za leseni kila mwaka Pamoja na ushuru kwa kuzingatia sheria ndogo za halmashauri.
Ewe mfanyabiashara ambaye unadaiwa hakikisha umelipa madeni yako kuepuka usumbufu, fika ofisi za Biashara eneo la Sekei chumba Na. 14.
LIPA KODI KWA WAKATI KWA MAENDELEO YA ARUSHA DC
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.