• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

TASAF YAENDELEA KUIMARISHA MAISHA YA KAYA MASIKINI ARUSHA DC

Posted on: February 18th, 2021

Na.Elinipa Lupembe.

Serikali imeendelea kuimarisha maisha ya wananchi wenye kipato cha chini, kupitia ruzuku ya fedha zinazotolewa kwa wananchi masikini, walio kwenye mpango wa Kunusu Kaya Masikini, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF awamu ya III.

Hayo yamethibitishwa wanufaika wa mpango wa kunusu kaya masikini Halmashauri ya Arusha, walipozungumza na mwandishi wetu, wakati wa zoezi la kupokea  ruzuku za wanakaya katika kijiji cha Oloirien kata ya  Oloirieni, zoezi lililofanyika kwenye ofisi ya kata ya Oloirieni.

Wanakaya hao wamesema kuwa, kabla ya kupokea fedha hizo za ruzuku kutoka TASAF, maisha yalikuwa magumu sana, huku baaadhi ya wanakaya kuthibitisha kushindwa kumudu kupata mahitaji ya muhimu ya familia kama malazi, chakula na mavazi na kuongeza kuwa fedha hizo zimewasaidia kumudu kupata mahitaji ya familia pamoja na kupata mahitaji ya shule kwa watoto, kwa kuanzisha miradi midogo ya kilimo na mifugo tafauti na hapa awali kabla ya neema ya mpango wa TASAF kuwashukia.

Leonia Nestori (64) mkazi wa kijiji cha Oloirieni na mnufaika wa mpango huo, amethibitisha kuwa fedha hizo za ruzuku ya TASAF zimemuwezesha kumudu kujikimu kimaisha, yeye na wajukuu zake ambao, amelazimika kuishi nao mara baada ya wazazi wao kufariki dunia na kubaki yatima.

"Mimi TASAF imenisaidia sana katika kuendesha maisha ya familia yangu, fedha ninazopokea zimenisaidia kununua mahitaji ya  shule ya wajukuu zangu, ambao ni yatima, kabla ya TASAF wajukuu zangu wangeweza hata kuacha shule, nilishindwa hata kuwanunulia nguo, kalamu, daftari na mahitaji mengine ya shule, kwa kweli, tunamshukuru Rais wetu Magufuli, ametuokoa sisi masikini" ameweka wazi Leonia. 

Aidha imeelezwa kuwa, kupitia fedha hizo za ruzuku, baadhi ya kaya masikini zimeweza kuanzisha miradi midogo midogo ya ujasiriamali, kilimo na ufugaji, miradi ambayo imewawezesha kupata fedha za kujikimu, kutokana na mazao wanayoyapata kutokana na mifugo na kilimo.

Loisojake Sangeti (74) mkazi wa Olosiva, amesema kuwa, kabla ya mradi huo wa TASAF, maisha yalikuwa magumu sana, lakini sasa TASAF imewezesha kaya nyingi kujikimu kimaisha kwa kutumia fedha hizo kununua kuku, mbuzi, kondoo na kuanza ufugaji, mifugo iliyowafanya kuwa na uhakika wa kupata chakula cha familia, pamoja na kununua mahitaji mengine muhimu kutokana na kuuza mifugo na mazao ya mifugo hiyo kama maziwa na mayai.

Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Saad Mtambule, amewataka wanakaya hao walioko kwenye mapango wa kunusuru Kaya masikini na wanaopokea ruzuku hiyo, kutumia fedha hizo vizuri kwa kuzingatia, lengo lililokusudiwa na serikali la kupambana na umasikini uliokithithiri sambamba na kuhakikisha kaya hizo zinaweza kujikimu kwa kupata mahitaji ya muhimu ya familia zao.

"Serikali inatoa pesa hizo kwa ajili ya ruzuku ya msingi ya kujikimu, ruzuku ya elimu kwa ajili watoto wanaosoma, kuwapatia mahitaji yao ya shule na kuhakikisha wanahudhuria shuleni bila kukosa, pamoja na ruzuku ya afya kwa watoto wa chini ya miaka mitano, kuhakikisha wanawapeleka kliniki na kupata huduma stahiki za afya ili kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano". Amesisitiza Mkurugenzi Mtambule.

Mratibu wa TASAF, halamshauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa jumla ya shilingi milioni 423.1 zinatarajiwa kugawiwa kwa kaya 8,223, kwenye vijiji 45 vilivyo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini, ikiwa ni ruzuku ya kipindi cha  miezi miwili.Awali jumla ya kaya 9,107 zilikuwa kwenye mpango wa kunusu kaya masikini Halmashauri ya Arusha, huku jumla ya wanakaya 79 kuondolewa kwa kufariki dunia, kaya 55 kuhama maeneo yao ya awali, kaya 4 kupoteza sifa kwa kuwa viongozi wa seriali, kaya 15 kujitoa kwenye mpango kwa hiari, kwa kuwa tayari zimejiweza na jumla ya kaya 541 hazikuhudhuria kwenye uhakiki awamu mbili zilizofanyika na kubakia kaya 8,223 ambazo zimepokea ruzuku awamu hii.


Mwezeshaji akimlioa fedha mnufaika wa kaya masikini kwenye kijiji cha Oloigueruno kata ya Olturoto.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.