Na Elinipa Lupembe.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, kupitia Mpango wa Kunusuru kaya Masikini, umekuwa na programu ya wanufaika wa mpango kuunda vikundi vya kuweka, kuwekeza na kukopa lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kujiinua kiuchumi kupitia vikundi hivyo.
Kama ilivyo kawaida ya vikundi vingine vya kuweka na kukopa, wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini kijiji cha Mungushi kata ya Bwawani, wamefanikiwa kuwa na kikundi imara kilichoanza miaka mitatu iliyopita.
Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kukutana na wanakikundi hao, siku ya malipo ya ruzuku ya mwezi 7/8, na kuzungumza na wanufaika hao, ambao wameweka bayana kuwa, walianzisha kikundi chenye jumla ya wanakikundi 15 na kukipa jina la CHIPUKIZI GROUP, kikundi ambacho kimewawezesha kuongeza kipato cha kaya, kinachowawezesha kumudu kupata mahitaji muhimu ya kaya zao.
Katibu wa kikundi cha CHIPUKIZI, Grace Sayale, amesema kuwa walipata mafunzo ya uundaji wa vikundi vya kuweka, kuwekeza na kukopa kutoka kwa wawezeshaji wa TASAF, na kuamua kujiunga kwenye kikundi na kuanza kuweka fedha na kukopeshana kwa riba ya asilimia 5 na hukutana kila wakati wa malipo ya ruzuku ya TASAF.
Aidha Grace ameishukuru Serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha kifedha, kwa kuwa hapo awali maisha yalikuwa magumu kwao na familia zao, kwa sasa kina mama wengi wameamka kiakili na kifkra, kila mwanamke anapambana kuwa na shughuli inakayomuingizia kipato tofauti na zamani.
"Kikundi kimetusaidia kukutana na kubadilishana mawazo ya kimaendeleo, wamama wengi wameamka na hata wasio walengwa wa TASAF, wanafanya kazi za kuingiza kipato, hakuna mwanamke siku hizi ana muda wa kupiga umbeya, zaidi tunajivunia kuwa na Rais mwanamke naye ametufanya tujiamini zaidi" Amefafanua Grace
Naye Mweka Hazina wa Kikundi cha CHIPUKIZI, Paulina Thomas, amefafanua kuwa, wao kama wanakikundi wana malengo ya kufika mbali kiuchumi, hivyo wanatumia pesa za ruzuku wanazipata kupitia TASAF kuweka na kukopa na kufanyia miradi midogomidogo ya ujasiriamali, kilimo na ufugaji.
"Tumewekeana mikakati kabla ya kumkopesha mwanakikundi, tunahakikisha ana malengo na kutuchanganulia matumizi ya fedha hiyo na mipango ya urejeshaji, ili mtu asikope pesa bila malengo" Amefafanua Mweka Hazina Paulina
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini, unaendelea kutekeza miradi mbalimbali, lengo likiwa ni kwejengea uwezo wanakaya wa kujikimu kimaisha, unaokwenda sambama na maendeleo ya kijamii katika sekta za afya, elimi na uchumi wa kaya.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
PICHA ZA KIKUNDI CHA CHIPUKIZI SIKU YA KUWEKEZA
Wanakikundi cha Chipukizi Group' wakiwa kwenye shughuli za kikundi za kukusanya pesa ya wekeza kwenye ofisi ya kikiji cha Mungushi mara baada ya kupokea ruzuku ya fedha za TASAF kwa mwezi 7/8 2022
Wanakikundi wa Chipkizi group wakikusanya fedha za kuwekeza.
Katibu wa Kikundi cha Chipukizi Grace Sayale ( wa kwanza kushoto) akiweka akiandika muhitasari kwa ajili ya kumbukumbu za kikundi na Mweka Hazina wa Kikundi Paulina Thomas (wa kwanza kulia) akihesabu fedha za makusanya ya kikundi.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.