Na. Elinipa Lupembe.
Wananchi wanaonufaika na fedha za ruzuku za mpango wa kunusuru kaya masikini, mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Maendeleo ya Jamii - TASAF, wamekiri fedha hizo kuwanufaisha katika kupunguza makali ya maisha pamoja na kujikwamuua kiuchumi na kijamii, huku fedha hizo zikiwawezesha wazazi wengi wenye watoto wanaosoma shule za kutwa, kulipia gharama za chakula cha mchana..
Wanakaya hao wa kijiji cha Ekenywa kata ya Olturumet, halmashauri ya Arusha, walio kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini, wameyasema hayo walipozungumza na mwandishi wetu, wakati wa zoezi la kupokea fedha hizo za ruzuku kwa kipindi cha miezi miwili ya Januari na Februari 2021, malipo yaliyofanyika kwenye shule ya msingi Ekenywa.
Wamesema kuwa, licha ya kuzitumia fedha hizo kujipatia mahitaji muhimu ya nyumbani na kuanzisha miradi midogo midogo, fedha hzio pia zimewawezesha kuwalipia watoto wao chakula cha mchana shuleni, kwa kuwa watoto wao wanasoma shule ambazo, wanatakiwa kuchangia chakula cha mchana kulingana na sera ya elimu ya mwaka 2015.
Martha Loishiye Mollel, mnufaika wa Mpango wa kunusu kaya maaikini, mama anayelea wajukuu wawili, ameekiri kuwa pindi anapopokea pesa za TASAF, licha ya kuzitumia kwa matumizi ya nyumbani, pesa hizo pia huzitumia kuwalipia wajukuu zake pesa za chakula cha mchana shuleni kama sera ya elimu inavyoelekeza.
"Kama wazazi tunatakiwa kuwalipia watoto wetu chakula cha mchana wawapo shule, pesa nilizopokea leo, nimetumia kiasi kidogo kuwalipia wajukuu zangu chakula cha mchana, nanafurahi kwa kuwa nilikiwa na deni, nilikuwa nadaiwa shilingi elfu 15, leo mnimelipa, sasa wajukuu zangu watasoma kwa amani". Amesisitiza Martha.
Naye Mariam Peter, mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Osiligi, amesema kuwa kaya yao hupokea fedha za ruzuku ya TASAF na mara nyingi huzitumia kununulia chakula pamoja kununua mahitaji yao ya shule, lakini pia hutumia kwa kulipia chakula cha mchana shuleni.
"Sisi tupo watoto watatu, mama yetu ni mgonjwa na baba anaishi nchini Kenya, huja nyumbani mara chache, pesa hizi zinatusaidia sana, nikipokea huwa tunanunua chakula, na pesa hizi nilizopkea leo nitamalizia kulipa fedha ya chakula shuleni, kukamilisha deni la muhula wa kwanza ambao tunalipa shilingi elfu 50 kwa muhula". Amefafanua Mariam.
Hata hivyo mwenyekiti wa Kitongoji cha Ekenywa, mheshimiwa Wilson Piniel Mollel, amesema kuwa kijiji chake kina kaya 482 zilizo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini, ameishukuru serikali kupitia mradi wa TASAF kwa kuwa ruzuku hiyo, licha ya kuwawezesha wananchi wake kujikwamua kiuchumi, kwa kujipatia mahitaji ya muhimu lakini pia kaya hizo maskini, zimeweza kumudu kuwalipia watoto wao walioko shuleni chakula cha mchana na kuwafanya watoto hao kusoma kwa amani na utulivu na kuongeza kuwa kama sio TASAF watoto wengi wangeshindwa kupata chakula cha mchana.
Mwalimu wa chakula, shule ya msingi Ekenywa, mwalimu Ema Mashana, amethibitisha kuwa wazazi wanopekea fedha za TASAF, huwalipia watoto wao chakula cha mchana wawapo shuleni, na mara nyingi pindi wanapopokea fedha hizo hulipa, na kwa kuwa malipo hufanyikia shuleni hapo, inakuwa rahisi wao kutoa fehda hizo.
Aidha amefafanua kuwa, wazazi kupiti Kamati ya shule walikubaliana kila mzazi kuchangia sado 5 za mahindi na sado 2 za maharagwe sado 2 kwa mwaka, (kipimo kisischo rasmi) na kwa wazazi wasiokuwa na mazao hayo hulazimika kulipia kiasi cha shilingi 10 kwa ajili ya maharagwe na shilingi efu 11 kwa mahindi kwa mwaka.
Awalii halmashauri ya Arusha, imepokea fedha kiasi cha shilingi milion 319, kutoka serikali kuu kupitia Mfuko wa Taifa wa Maendelo ya Jamii -TASAF, mradi wa Mpango wa Kunusu Kaya masikini, ikiwa ni fedha za ruzuku kwa kaya masikini, kwa kipindi cha mwezi Januari na Februari, 2021, huku jumla ya kaya 8,167 zikunufaika na fedha hizo, kutoka vijiji 45 vya halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.