Mnufaika wa Mpango wa TASAF, Bi. Christina Johnas kutoka Kitongoji cha Songambele, Kijiji cha Themi ya Simba, Kata ya Bwawani, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, ameonesha furaha yake kutokana na mafanikio aliyoyapata kupitia mpango huo.
Bi. Christina amesema kuwa tangu kuanza kupokea ruzuku ya uzalishaji kupitia programu ya kukuza uchumi wa kaya, amekuwa akipata faida kubwa. Mpaka sasa, amefanikisha kupata milo mitatu kwa familia yake kila siku, pia ana mbuzi na kuku, na ana uwezo wa kumsaidia mtoto wake kusoma bila vikwazo.
“Mpango wa TASAF umenisaidia sana. Sasa familia yangu ina chakula cha kutosha na ninaweza kumsaidia mtoto wangu kupata elimu bora,” amesema Bi. Christina.
Aidha, Bi. Christina aliongeza shukrani zake kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wafadhili wa mpango huo, kwa kuwajengea kaya masikini kituo cha afya kilichopo kijiji cha Themi ya Simba, jambo ambalo limeongeza faraja na ustawi wa wananchi wa kijiji hicho.
Mpango wa TASAF una lengo la kuwasaidia kaya masikini kupitia ruzuku za uzalishaji na mipango ya maendeleo ya jamii, ambapo wagombea wanapata fursa ya kujenga uchumi thabiti na kuondokana na umasikini.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.