Timu ya Wataalam wa masuala ya Utafiti wa Afya ya udongo toka Wizara ya Kilimo yatua Mkoani Arusha kwajili ya tafiti za masuala ya kilimo.
Ziara hiyo ya Kitafiti ina lengo la kuweza kuainishi aina ya udongo na aina gani sahihi ya mbolea inayopaswa kutumiwa na wakulima, kwani miaka ya hivi karibuni baadhi ya wakulima wamekuwa wakitumia mboleo pasipo kuzingatia elimu ya tafiti za afya udongo.
Akizungumza katika kikao hicho,Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Kilimo Mhandisi Makoli Godwini amesema zoezi la upimaji wa Afya ya udongo ni la Nchi nzima na lilianzia Mkoa wa Ruvuma na sasa wapo Mkoa wa Arusha.
Amesema zoezi hilo linahusisha kuchukua sampuli za udongo kwenye maeneo tofauti kwenye Kata mbalimbali ndani ya Mkoa wa Arusha na kuzipeleka maabara na matokeo ya tafiti hizo yatarejeshwa kwa Wakulima na Wafugaji ili ziweze kuwasaidia katika kujua aina gani ya mbolea ifaayo kutumika katika shughuli zao za kilimo.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha,bwana Seleman Msumi amepongeza hatua ya Serikali chini ya Wizara ya Kilimo kwa kuja na mpango wa kuwasaidia Wakulima na Wafugaji kwa kufanya tafiti zitakazo leta matokeo chanya katika uzalisha wa mazao ya biashara na chakula.
" Mpango unaenda kuwa suluhisho la mkulima kuhangaika na matumizi holela ya mbolea, kwani ilifika mahala mkulima anatumia mbolea bila kujua aina gani ya mbolea inafaa kwa udongo upi,,kitu hiki kilisababisha watu wetu kupata mazao hafifu." Alisema Msumi.
Zoezi hilo linaanzia katika Halmashauri ya Arusha kwa kuzitembelea Kata mbalimbali na kuchukua sampuli ya udongo kisha litaendelea katika Halmashauri nyinginezo za Mkoa wa Arusha kabla ya kwenda Mikoa ya Kilimanjaro na Manyara.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.