TRC YAKUSUDIA KUJENGA RELI YA KISASA (SGR) KWA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI.
(Jumanne, Machi 25, 2025 – Arusha)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa ofisini kwake kuhusu mpango wa ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway) itakayounganisha mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Katika kikao hicho, Bw. Kadogosa alieleza kuwa Serikali inatarajia kuanza mchakato wa ujenzi wa reli hiyo, mradi unaotekelezwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kama sehemu ya maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ujenzi huu unalenga kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kukuza uchumi wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini na mikoa jirani.
Akizungumza kuhusu manufaa ya mradi huo, Bw. Kadogosa alisema kuwa reli hiyo ya kisasa itakuwa chachu ya maendeleo kwa mikoa ya kanda ya kaskazini Arusha ukiwa mmoja wapo hasa katika sekta ya uchukuzi, usafirishaji,Utalii, biashara na madini. Alifafanua kuwa uwepo wa madini ya Magadi soda eneo la Engaruka na bonde la Ziwa Natron katika mkoa wa Arusha imekuwa chachu ya ujenzi wa mradi huo, huku akibainisha kuwa machimbo ya madini hayo yana uwezo wa kudumu kwa zaidi ya miaka mia moja.
Aidha, alieleza kuwa ujio wa bomba la mafuta kutoka Hoima- Uganda hadi Chongoreani-Tanga utahitaji mfumo madhubuti wa usafirishaji wa mafuta ghafi, na reli hii itakuwa njia mojawapo muhimu ya kusafirisha mafuta hayo hadi masoko ya mataifa mengine katika Afrika.
Kwa upande wake, Mhe. Makonda alimshukuru Rais Samia kwa uwekezaji mkubwa unaofanyika katika Mkoa wa Arusha, akiahidi kuwa wakazi wa mkoa huo wataendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazoletwa na serikali ya awamu ya sita.
Pia, Makonda alisisitiza kuwa Arusha imejipanga kuweka rekodi kwa idadi kubwa ya kura kwa Rais Samia katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu kama ishara ya shukrani kwa miradi inayotekelezwa, ikiwemo ukuzaji wa uchumi, uimarishaji wa sekta ya utalii, madini, na kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara.
Ikumbukwe kuwa Nchi jirani ya Kenya kwa miaka mingi inatekeleza mradi mkubwa wa uchimbaji,uzalishaji na usafirishaji wa madini ya magadi soda
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.