TUMEKAMILISHA UJENZI WA VYUMBA 2 VYA MADARASA SEKONDARI LOSINONI
Na Elinipa Lupembe
Shule ya sekondari Losinoni tumekamilisha ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 40 fedha kutoka Serikali Kuu.
Kiasi hicho cha fedha kimejumuisha ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, ofisi ya walimu, viti na meza za wanafunzi 50 kwa kila darasa, ikiwa ni mradi maalum kwa maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, watakaopangiwa kwa mwaka wa masomo utakaoanza Januari 2023.
Awali Serikali imetoa shilingi milioni 760 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 38 kwa 18 za sekondari, halmashauri ya Arusha kwa maandalizi ya kidato cha kwanza 2023.
ARUSHA DC
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.