Na Elinipa Lupembe
Ukarabati wa kituo cha Walimu -TRC Naurei kata ya Kiutu, umekamilika, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 22 fedha kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji kupitia mradi wa GPE - LANES II.
Serikali imefanya ukarabati wa vituo vya walimu nchini, kufuatia mpango wa Serikali wa kuboresha miundo mbinu ya Elimu msingi nchini, kwa lengo la kuimarisha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ( KKK).
Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Mwl. Salvatory Alute, amesema kuwa, kukamilika kwa mradi huo, kutawawezesha walimu kupata mafunzo kazini, mafunzo ambayo yatawajengea uwezo wa kujiongezea maarifa ya ufundishaji, hali itakayowezesha wanafunzi kujifunza stadi tatu za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Awali, halmashauri ya imetekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vitano vya walimu kwa gharama ya shilingi milioni 110, kufuatia mpango wa serikali wa kuboresha miundo mbinu ya Elimu msingi nchini, ili kuimarisha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ( KKK).
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.