• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

UFAULU WA ILBORU WAWEZESHA KUPATA KOMPYUTA ZA TCRA

Posted on: November 22nd, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzani (TCRA), imeendelea kuimarisha miundombinu ya TEHAMA kwenye shule zinazoshika nafasi za juu kitaifa nchini, kwa kutoa motisha ya seti za Kompyuta kwenye shule hizo.

Shule ya sekondari Ilboro, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru ni miongoni mwa shule tano bora, zilizonufaika na mpango huo, kwa kupata seti komputa kumi na kutengenezewa tovuti ya shule, kwa kuweza  kukidhi vigezo hivyo vilivyowekwa na TCRA, vifaa vitaksvyotumika kujifunzia somo la TEHAMA kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega licha ya kuishukuru TCRA kwa msaada huo wa Kompyuta, amewapongeza  walimu na wanafunzi kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa, na kuwataka walimu na wanafunzi kuvitunza vifaa hivyo, pamoja na kuvitumia kwa matumizi sahihi ya kujifunzia kama  iliyokusudiwa na Serikali.

Ameeleza kuwa, kwa miaka minne mfululizo shule za mkoa wa Arusha zimekuwa zikifanya vizuri na kuufanya mkoa wa Arusha, kuingia kwenye kumi bora katika mitihani ya madarasa yote yanayofanya mitihani ya taifa, ikiwemo darasa la nne na la saba, kidato cha pili, cha nne na cha tano.

Ameongeza kuwa, anategemea sasa shule ya Ilboru, itafanya vizuri zaidi na kushika nafa si ya kwanza, kutokana na urahisi wa kujifunza kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia Kompyuta hizo.

"Kama wakati wa analojia, Iboru ilikuwa kwenye shule tano bora, kupitia teknolojia ya dijitali, sasa Ilboru itakuwa Tanzania one" amesema Katibu Tawala huyo.

Naye Mkurugenzi wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Imelda Salum, amesema kuwa TCRA, imetoa vifaa hivyo vya kujifunzia kwa lengo la kuwajengea wanafunzi  uwezo wa kutumia  kompyuta kwenye masomo yao na kurahisisha tendo la kujifundisha na kujifunza.

Ameongeza kuwa, licha ya kuwa jukumu la TCRA ni kuhakikisha wananchi wote wanapata mawasiliano, lakini  pia wana mkakati wa kutoa vifaa vya TEHAMA kwenye sekta ya elimu, ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kutumia teknolojia hiyo wangali shuleni.

Aidha, Mhandisi Imelda ametaja vifaa walivyokabidhi shuleni hapo ni pamoja na seti kumi za compyuta za mezani ikiwemo 'monitor, serve na printer'pamoja na kutengeneza tovuti ya shule hiyo, ambayo itawezesha kuweka taarifa zote muhimu za shule, ikiwemo matokeo ya wanafunzi.

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye, ameahidi kusimamia matumizi sahihi ya Kompyuta hizo na kuwataka walimu kuhakikisha zinawewezesha wanafunzi kupata maarifa ya msomo yao na kujifunza mambo ya msingi kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla na si vinginevyo.

"Tunafahamu mitandao ina taarifa nyingi mnoo, ni jukumu letu walimu, kuwaongoza na kuwasimamia wanafunzi, kutumia kwa mambo ya msingi na ya muhimu katika maisha yao, wanafunzi wekezeni muda wenu kujifunza mambo ya muhimu na si vinginevyo" amesisitiza mkurugenzi huyo.

Hata hivyo wanafunzi wa sekondari Ilboru, licha ya kuishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, wamesema kuwa wanatambua juhudi  kubwa zinazofanywa na Serikali ya sasa, za  kuboresha na kuimarisha miundombinu ya kujifunzia kwenye shule za serikali na kuongeza kuwa, Komputa hizo, zitawarahisishia tendo la kujifunza, jambo ambalo litapandisha taaluma yao pamoja na  kuongeza kasi ya ufaulu kwa shule yao.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Ilboru, mwalimu Denis Otieno, ameishukuru Serikali, kupitia TCRA kwa msaada huo mkubwa, ambao utawezesha wazazi/walezi, wanafunzi na jamii, kupata taarifa za shule ya Ilboru popote walipo kupitia tovuti ya shule, iliyotengenezwa na mamlaka hiyo.

Mpaka sasa jumla ya shule za sekondari 20 za serikali, halmashauri ya Arusha, zina maabara za Kompyuta jambo ambalo linaendelea kupandisha kwa kasi taaluma na kupanda kwa kiwango cha ufaulu kwa shule za serikali tofauti na hapo awali.


Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.