UFUNGUZI WA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE KANDA YA KASKAZINI
Posted on: August 5th, 2025
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga mapema hii leo Agosti 5, 2025 amekagua mabanda mbalimbali katika maonesho ya Wakulima nane nane na kujionea shughuli mbalimbali, ikiwemo za Kilimo na Mifugo Na Uvuvi.
Maonesho hayo ya Kanda ya Kaskazini yaliyoanza Agosti Mosi, 2025 yanafanyika katika viwanja vya Themi vilivyopo Njiro jijini Arusha na yamezinduliwa rasmi hii leo Agosti 5, 2025 na mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu huyo wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga.