Na Elinipa Lupembe
Ujenzi wa Kituo cha walimu Klasta ya Ilkurot kata ya Lengijave umeanza ukiwa katika hatua za awali za msingi.
Ujenzi huo utakaogharimu shilingi milioni 20, fedha kutoa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu kupitia miradi ya GPE - LANES II, unategemea kukamilika baada ya miezi mitatu kuanzia sasa.
Hata hivyo ujenzi huo unatumia force Account kwa mujibu wa maelekezo huku fedha hizo zikielekezwa katika ukamilishaji wa majengo yote pamoja na ununuzi wa samani zake ikiwa ni pamoja na viti na meza 45.
Aidha mradi huo ni miongoni mwa miradi 5 ya ujenzi wa vituo vya walimu, vinayojengwa katika halmashauri ya Arusha baada ya serikali kutoa shilingi milioni 110 lengo likiwa ni kuboresha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa shule za Msingi.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.