Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango leo ameitimisha Mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwenye hafla iliyofanyika Kata ya Bwawani Halmashauri ya Arusha.
Katika hafla hiyo jumla ya vijana 92 kata ya vijana 147 waliandikishwa kuanza mafunzo hayo tarehe mapema mwezi Agosti, 2022 huku wanawake wakiwa 10 na wanaume 82.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru amewaasa vijana wote waliomaliza mafunzo hayo, kuwa watii na wazalendo kwa Taifa lao na kuhakikisha wanatumia maarifa waliyoyapata kuendeleza amani na utulivu katika nchi hii.
Aidha amewakumbusha utii kwa viongozi wote na kwa kuwa Mhe.Rais Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka mfumo mzuri wa majeshi ya Ulinzi na wao kwa sasa ni sehemu ya Ulinzi wa Taifa.
"Tumieni mafunzo haya kulitumika Taifa na zaidi katika kulinda raia na mali zao na siyo kuvunja sheria za nchi, kwa serikali imewaamini na kuwapa mbinu za ulinzi na usalama wa raia, hiyo jukumu lenu kubwa ni kuwatumikia wananchi". Amesema Mkuu huyo wa Wilaya
Mkufunzi wa Mgambo Wilaya ya Arumeru Meja Khamis licha ya kumshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kukubali kuja kufunga Mafunzo hayo amewapongeza wakufunzi wote waliofanikisha Mafunzo ikiwa ni pamoja na kuitaka jamii kuwapa vijana hao ushirikiano pindi watakaporudi katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa, vijana hao 92 pamoja na mafunzo ya Kijeshi waliopata, walipata pia mafunzo kutoka Jeshi la Uokoaji na Zima Moto, Takukuru, Mafunzo ya Kareti, Mafunzo ya Jeshi la Uhamiaji na Mafunzo ya Kupambana na Dawa za Kulevya, mafunzo ambayo yamewapa mbinu na maarifa ya ulinzi wa raia na mali zao.
Wakisoma Risala yao kwa mgeni sasmi, vijana hao wameiomba serikali kuupa fursa ya mafunzo hayo mara kwa mara ili kukuza na kuendeleza maarifa na ujuzi katika kazi.
Aidha wakaiomba serikali kuwaunganisha na mashirika na makampuni ya ulinzi ili waweze kupata ajira pamoja na kuwapa kipaumbele kwenye kazi maalumi za serikali kama vile uchaguzi, wakati wa mitihani.
Hata hivyo, Taasisi za Ulinzi zikiongozwa na SUMA JKT Sajenti Ndege, amemuahidi mkuu wa wilaya kuwachukua vijana 50 ili kuwapatia ajira kwenye kampuni ya SUMA JKT inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa.
Katika sherehe hizo mkuu wa wilaya aliambatana nawajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, viongozi wa halmashauri za Arusha na Meru, viongozi wa Chama, viongozi wa dini na wa siasa pamoja na wananchi wa halmashauri zote mbili
ARUSHA DC
KaaiInaendelea ✍
PICHA ZA MMATUKIO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.