Vijana Halmashauri ya Arusha, wameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa kuwapa vijana mikopo isiyokuwa na riba kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri zao.
Wakizungumza mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi @comred_suma vijana watano wa Kikundi cha cha Shine Youth Group, wameishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo isiyokuwa na riba na kukabiliana na changamoto ya ajira.
Katibu wa kikundi hicho, Steven Mashuve amesema kuwa kikundi hicho kilichopo kata ya Mlangarini kijiji cha Kiseriani kinajishughulisha na utengezaji samani, kilianza kwa kusuasua kwa mtaji wa ahilingi milioni 1.2 na baada ya kupewa mkopa shilingi milioni 10 licha ya kuanza kurejesha mkopo lakini bado wanapata faida ya biashara yao.
"Tunamshukuru Rais wetu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha kwa kutupa mkopo wa shilingi milioni 10, umetuwezesha kukuzamtaji wetu wa kutengeneza na kuuza samani za ndani, kazi ambayo ndio inatusaidia kuimarisha uchumi wetu na familia zetu huku tukipata fedha za kujikimu kimaisha".Wamesema vijana hao
Akizungumza mara baada ya kukagua na kuridhishwa na mradi huo, Ndugu Ussi amewapongeza vijana hao kwa kichangamkia fursa na kupata mikopo isiyokuwa na riba ya 10% inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani na kuifanyia kazi huku wakirejesha kwa wakati.
Aidha, amewasisitiza vijana wengine kuiga mfano wa vijana hao, kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo inayotolewa na Serikali, mikopo ambayo haipatikani kwenye taasisi nyingine za kifedha.
KAULI MBIU: "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa Amani na Utulivu"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.