Na. Elinipa Lupembe.
Vijana halmashauri ya Arusha wameamua kujikita, kwenye shughuli za ujasiriamali ili kupambana na hali ngumu ya maisha inayowakabili, kutokana na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira iliyowakumba vijana wengi kwa sasa.
Kufuatia changamoto hiyo, jumla ya vijana 70 wenye nia ya kuwa wajasiriamali, kutoka kata 27 za halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuwa na malengo, yanaotekelezeka huku wakijikita zaidi, kuangalia fursa na mahitaji ya jamii inayowazunguka katika maeneo yao.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa mradi kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya Vissio For Youth, Vedastus Sigula, wakati akitoa mafunzo ya siku moja kwa vijana hao, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Arusha.
Meneja huyo amefafanua kuwa ili kuwa mjasiriamali ni lazima kuwa na malengo yanayotekelezeka na baada ya malengo ni kuzitazama fursa ndipo una wazo la biashara.
"Jambo la kwanza kwa mjasiriamali ni kuwa na lengo linalotekelezeka, pili angalia fursa zinazokuzunguka kwenye eneo lako ndipo utoke na wazo la shughuli unayotaka kufanya, hapo unaweza kufanikiwa" amesema Sigula.
Hata hivyo vijana hao, baada ya kupata mafunzo hayo wameonyesha kupata mwanga juu ya ujasiriamali tofauti na mawazo waliyokuwa nayo kabla ya mafunzo.
Stela Lomayani wa kijana wa kata ya Mwandeti, amesema kuwa hakufahamu kama ujasiriamali una misingi yake ya kufuata huku akijipambambanua kuwa sasa ana uwezo wa kuweka malengo, kuchagua fursa, kuandaa andiko la mradi pamoja na kuweka mipango ya kusimamia mradi huo.
"Nimejifunza namna ya kuweka malengo, si malengo tuu, malengo yanayotekelezeka, kupambanua fursa, kutengeneza business plan, jinsi ya kusimamia mradi kwa kuweka records za biashara" amesema Stella.
Naye Elipokea Ayo kijana kutoka kijiji cha Oldonyowas amethibitisha kutambua, jinsi ya kuanzisha biashara inayoendana na mazingira na wakati husika huku akiwataka vijana wenzie kutokukata tamaa kwa kukosa ajira badala yake kutumia fursa nyingi zinazopatika katika maeneo yao.
Awali akifungua mafunzo hayo, Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, amewataka vijana hao, kutumia fursa hiyo ya mafunzo kuwa na bidii katika kuendesha biashara ili kupambana na changaomto ya ajira inayowakabili vijana wengi kwa sasa.
Asasi ya Vission for Youth, imejipanga kutoa mafunzo ya kibiashara kwa zaidi ya vijana 200 kwenye halmashauri ya Jiji la Arusha na zile za wilaya ya Arumeru, kwa lengo la kuwapa mbinu za ujasiriamali na kuwawezesha kuandika andiko la mradi, kwa vijana watakao andika vizuri atapewa mkopo wa riba nafuu pamoja na kusimamiwa mpaka vijana hao watakapokuwa na uwezo wa kusimamia biashara.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.